-
Je, Kweli Yesu Alikufa Juu ya Msalaba?Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
-
-
Tangu wakati huo, misalaba yenye maumbo na miundo mbalimbali imetumiwa. Kwa mfano, kamusi fulani ya Biblia (The Illustrated Bible Dictionary) inasema kuwa ule unaoitwa msalaba wa Mt. Anthony “ulikuwa na umbo linalofanana na herufi kubwa ya T. Watu fulani wanafikiri kuwa umbo la msalaba huo lilitokana na alama ya mungu Tamuzi [wa Wababiloni].” Pia kulikuwa na msalaba wa Mt. Andrew, ambao una umbo la herufi ya X, na ule msalaba tunaojua ambao una mbao mbili zilizokingamana. Msalaba huu wenye mbao mbili zilizokingamana unaitwa msalaba wa Kilatini, na “katika mapokeo unaonwa [kimakosa] kuwa aina ya msalaba ambao Bwana wetu alikufa juu yake.”
-
-
Je, Kweli Yesu Alikufa Juu ya Msalaba?Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
-
-
Kwa mfano, mara nyingi maandishi ya kale ya michoro ya Misri na pia michoro ya miungu yao, inaonyesha umbo la herufi T ikiwa na duara juu. Msalaba huo unaitwa ansate, au msalaba wenye kishikio, ambao unafikiriwa kuwa ishara ya uhai. Baada ya muda, msalaba huo ulikubaliwa na kutumiwa sana na Kanisa la Koptiki na makanisa mengine.
Kulingana na kitabu fulani cha marejeo (The Catholic Encyclopedia), “inaonekana msalaba wa zamani zaidi ni ule unaoitwa msalaba wa ‘gamma’ (crux gammata), ambao watu wa Mashariki na wanafunzi wanaochunguza vitu vya kale wanaujua kwa jina lake la Kihindi cha zamani, swastika.”
-
-
Je, Kweli Yesu Alikufa Juu ya Msalaba?Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 19]
Mchoro wa ukutani wa Wamisri (yapata karne ya 14 K.W.K.) Unaoonyesha msalaba wa ansate, ishara ya uhai
[Hisani]
© DeA Picture Library / Art Resource, NY
[Picha katika ukurasa wa 19]
Msalaba wa gamma kwenye Hekalu la Laxmi Narayan la Wahindu
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 20]
From the book The Cross in Tradition, History, and Art (1897)
-