Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ngome ya Terezín—Haikuweza Kuzuia Mateso
    Amkeni!—2012 | Machi
    • Mashahidi wa Yehova 20 hivi kutoka Prague, Pilsen, na sehemu nyingine nchini humo walifungwa katika Ngome hiyo Ndogo. Walikuwa wamefanya kosa gani? Walikataa kuwategemeza Wanazi na hawakuunga mkono upande wowote katika siasa. Licha ya kazi ya kuhubiri kupigwa marufuku, Mashahidi waliendelea kuwaeleza watu wengine habari njema kutoka katika Biblia. Waliteseka kwa sababu tu ya imani yao, na wengine wakauawa au wakateswa hadi walipokufa.

  • Ngome ya Terezín—Haikuweza Kuzuia Mateso
    Amkeni!—2012 | Machi
    • [Sanduku katika ukurasa wa 20]

      MASHAHIDI WA YEHOVA KATIKA NGOME NDOGO

      Wengi wa Mashahidi wa Yehova waliofungwa huko Theresienstadt walihojiwa kwanza katika makao makuu ya Gestapo huko Prague. Kwa kawaida, walipotolewa Theresienstadt walipelekwa kwenye kambi za mateso huko Ujerumani. Walifauluje kukabiliana na hali ngumu gerezani na vilevile na kutengwa?

      Mwanamke fulani Shahidi ambaye alifungwa huko Theresienstadt anakumbuka hivi: “Kwa sababu sikutaka kusahau mafundisho ya Biblia, niliyarudia tena na tena. Katika kila gereza nililohamishwa, nilijaribu kuona kama kuna Mashahidi wengine; na nilipopata habari kwamba wako, nilijaribu kuwasiliana nao. Wakati huohuo nilijitahidi kuwahubiria watu kadiri hali zilivyoruhusu.”

      Njia yake ilifaulu. Aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu muda wote aliokuwa amefungwa na hata katika miaka iliyofuata.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki