Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tulitegemea Nguvu za Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Agosti 1
    • Simulizi la Maisha

      Tulitegemea Nguvu za Yehova

      LIMESIMULIWA NA ERZSÉBET HAFFNER

      “Sitawaruhusu wakuhamishe,” akasema Tibor Haffner aliposikia kwamba nilikuwa nimeamriwa niondoke Chekoslovakia. Kisha akaongeza kusema: “Ukikubali nitakuoa, kisha utabaki nami milele.”

      JANUARI 29, 1938, majuma machache tu baada ya kuniomba bila kutarajia niwe mke wake, niliolewa na Tibor, ndugu Mkristo ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuihubiria familia yetu. Huo haukuwa uamuzi rahisi. Nilikuwa tu nimefikisha umri wa miaka 18, na nikiwa mhudumu wa wakati wote wa Mashahidi wa Yehova, nilitaka kutumia miaka yangu ya ujana katika kumtumikia Mungu tu. Nililia na kusali. Baada ya kutulia nilitambua kwamba ombi la Tibor la kunioa lilihusisha mengi zaidi ya tendo la fadhili, nami nilihisi kwamba nilitaka kuishi na mwanamume huyo aliyenipenda kikweli.

      Lakini kwa nini nilikabili hatari ya kuhamishwa na hali niliishi katika nchi ambayo ilijivunia mfumo wake wa kidemokrasia na uhuru wa kidini?

  • Tulitegemea Nguvu za Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Agosti 1
    • Ingawa kazi yetu ilikuwa imeandikishwa rasmi, tulikabili upinzani mkali sana uliochochewa na makasisi.

      Twateswa

      Siku moja mwishoni mwa mwaka wa 1937, nilikuwa nikihubiri pamoja na dada mwingine Mkristo katika kijiji kimoja kilicho karibu na Lučenec. Baada ya muda mfupi, tulikamatwa na kupelekwa gerezani. “Mtafia hapa,” akasema mlinzi, huku akiufunga mlango wa seli kwa nguvu.

      Kufikia jioni, wanawake wengine wanne walikuwa wameletwa katika seli hiyo. Tulianza kuwafariji na kuwahubiria. Walitulia, nasi tukazungumza nao kweli ya Biblia usiku kucha.

      Saa kumi na mbili asubuhi, mlinzi aliniita nitoke kwenye seli. Nami nikamwambia mwenzangu: “Tutaonana tena katika Ufalme wa Mungu.” Nilimwambia kwamba ikiwa ataokoka aieleze familia yangu kilichotukia. Nilitoa sala fupi na kuandamana na mlinzi huyo. Alinipeleka nyumbani kwake katika eneo la gereza. “Msichana, ningependa kukuuliza maswali kadhaa,” akasema. “Jana usiku ulisema kwamba jina la Mungu ni Yehova. Je, unaweza kunionyesha jina hilo katika Biblia?” Nilishangaa na kuhisi nimetulia sana. Alileta Biblia yake, kisha nikamwonyesha yeye pamoja na mke wake jina Yehova. Alikuwa na maswali mengi kuhusu habari tuliyokuwa tumezungumzia pamoja na wale wanawake wanne usiku. Kwa kuridhishwa na majibu hayo, alimwomba mke wake atayarishe kiamsha-kinywa kwa ajili yangu na mwenzangu.

      Siku chache baadaye, tulifunguliwa, lakini hakimu mmoja akaamua kwamba kwa kuwa nilikuwa raia wa Hungaria, nilipaswa kuondoka Chekoslovakia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki