-
Tegemea Roho ya Mungu Unaposhughulika na Mabadiliko ya MaishaMnara wa Mlinzi—2004 | Aprili 1
-
-
Usiutumaini Utajiri Usio Hakika
15. (a) Watu fulani hutumiaje utajiri wao? (b) Daudi alitamani kutumia mali yake jinsi gani?
15 Hakuna jambo linaloonyesha kwamba Daudi alitoka katika jamii ya tabaka la juu au familia yenye mali. Hata hivyo, wakati wa utawala wake, Daudi alipata mali nyingi. Kama unavyojua, watu wengi hujirundikia mali, hujaribu kuiongeza kwa pupa, au kuitumia kwa ubinafsi. Wengine hutumia pesa zao kujitukuza. (Mathayo 6:2) Daudi alitumia mali yake kwa njia tofauti. Alitamani kumtukuza Yehova. Daudi alimweleza Nathani tamaa yake ya kumjengea Yehova hekalu ili kuliweka ndani sanduku la agano, ambalo wakati huo lilikuwa Yerusalemu ‘likikaa katikati ya vitambaa vya mahema.’ Yehova alipendezwa na yale ambayo Daudi alikusudia kufanya, lakini kupitia Nathani akamwambia Daudi kwamba Sulemani mwanaye ndiye angejenga hekalu hilo.—2 Samweli 7:1, 2, 12, 13.
16. Daudi alifanya matayarisho gani kwa ajili ya ujenzi wa hekalu?
16 Daudi alikusanya vifaa ambavyo vingetumiwa katika ujenzi huo mkubwa naye akamwambia Sulemani hivi: “Nimetayarisha kwa ajili ya nyumba ya Yehova talanta mia moja elfu za dhahabu na talanta milioni moja za fedha, na hakuna namna ya kupima uzito wa shaba na chuma kwa sababu zimekuwa nyingi sana; nami nimetayarisha mbao na mawe, lakini utaviongeza vitu hivyo.” Alichanga talanta 3,000 za dhahabu na 7,000 za fedha kutoka katika hazina yake mwenyewe.a (1 Mambo ya Nyakati 22:14; 29:3, 4) Daudi alitoa kwa ukarimu ili kuonyesha imani na ujitoaji wake kwa Yehova Mungu, wala si kujionyesha. Kwa kutambua Chanzo cha utajiri wake, alimwambia Yehova hivi: “Maana kila kitu hutoka kwako, nasi tumekupa kutoka katika mkono wako mwenyewe.” (1 Mambo ya Nyakati 29:14) Moyo mkarimu wa Daudi ulimchochea afanye yote awezayo ili kuendeleza ibada safi.
-
-
Tegemea Roho ya Mungu Unaposhughulika na Mabadiliko ya MaishaMnara wa Mlinzi—2004 | Aprili 1
-
-
a Kulingana na viwango vya leo, mchango ambao Daudi alitoa, una thamani ya zaidi ya dola 1,200,000,000 za Marekani.
-