Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yonathani “Alifanya Kazi na Mungu”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • MWANA wa mfalme wa kwanza wa Israeli anamtembelea mkimbizi mafichoni. “Usiogope,” anamwambia mkimbizi huyo, “kwa kuwa mkono wa Sauli baba yangu hautakupata, na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli, na mimi nitakuwa wa pili kwako.”—1 Samweli 23:17.

      Mwana huyo ni Yonathani, naye mkimbizi ni Daudi. Ikiwa Yonathani hangekufa muda mfupi baadaye, inawezekana kwamba angemtegemeza Daudi kabisa.

      Urafiki wa Yonathani na Daudi ulikuwa wa ajabu. Kwa kweli,

  • Yonathani “Alifanya Kazi na Mungu”
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • Yonathani na Daudi

      Miaka 20 hivi baadaye, Goliathi, shujaa Mfilisti alidhihaki jeshi la Waisraeli, lakini Daudi akamuua. Ingawa Yonathani alimzidi Daudi umri kwa miaka 30, wanaume hao wawili walilingana sana.a Ujasiri ambao Yonathani alionyesha huko Mikmashi ulionyeshwa pia na Daudi. Ulinganisho mkubwa zaidi kati yao ni kwamba, Daudi alikuwa na imani ileile katika nguvu za Yehova za kuokoa, imani iliyomwezesha kupambana na Goliathi bila woga wakati Waisraeli wengine wote walipojikunyata kwa woga. Kwa sababu hiyo, “nafsi ya Yonathani ikashikamana na nafsi ya Daudi, na Yonathani akaanza kumpenda kama nafsi yake mwenyewe.”—1 Samweli 17:1–18:4.

      Ujasiri wa Daudi ulimfanya Mfalme Sauli amwone kuwa mpinzani, hata hivyo, Yonathani hakumwonea Daudi wivu hata kidogo. Yonathani na Daudi walikuja kuwa marafiki wakubwa sana, na inaelekea kwamba kupitia mazungumzo yao ya siri, Yonathani alipata kujua kuwa Daudi alikuwa ametiwa mafuta awe mfalme wa Israeli ambaye angefuata. Yonathani aliheshimu uamuzi wa Mungu.

      Mfalme Sauli alipozungumza na mwana wake na watumishi wake kuhusu kumuua Daudi, Yonathani alimwonya Daudi. Yonathani alimsadikisha Sauli kwamba hakuwa na sababu ya kumwogopa Daudi. Daudi hakuwa amemtendea mfalme dhambi hata kidogo! Je, Daudi hakuhatarisha uhai wake kwa kumkabili Goliathi? Ombi la kutoka moyoni la Yonathani kwa ajili ya rafiki yake aliyekuwa amekosewa lilimtuliza Sauli. Hata hivyo, muda si muda mfalme alipanga tena njama ya kumuua Daudi naye alijaribu tena na tena kumuua, na hivyo Daudi akalazimika kukimbia.—1 Samweli 19:1-18.

      Yonathani alimuunga Daudi mkono kwa ushikamanifu. Marafiki hao wawili walikutana ili kupanga watakalofanya. Akiwa mshikamanifu kwa rafiki yake, huku akijitahidi kuwa mshikamanifu kwa baba yake, Yonathani alimwambia Daudi hivi: “Ni jambo lisilowaziwa! Hutakufa.” Hata hivyo, Daudi akamwambia Yonathani: “Kuna kama hatua moja tu kati yangu na kifo!”—1 Samweli 20:1-3.

      Yonathani na Daudi walipanga jinsi ya kujaribu nia ya Sauli. Ikiwa ingegunduliwa kwamba Daudi hayupo mezani pa mfalme, Yonathani angemwambia baba yake kwamba Daudi aliomba ruhusa ya kutokuwepo ili aende akashiriki kutoa dhabihu kwa ajili ya familia. Iwapo Sauli angekasirika, hiyo ingekuwa ishara ya kwamba alikusudia kumuumiza Daudi. Yonathani alimbariki Daudi na kwa njia isiyo ya moja kwa moja akamkubali kuwa mfalme atakayefuata, akisema hivi: “Yehova na awe pamoja nawe, kama vile alivyokuwa pamoja na baba yangu.” Marafiki hao wawili waliapa kuwa washikamanifu kwa mmoja na mwenzake na wakaamua jinsi ambavyo Yonathani angemjulisha Daudi kuhusu matokeo ya mpango wao.—1 Samweli 20:5-24.

      Sauli alipogundua kwamba Daudi hayupo, Yonathani alieleza kwamba Daudi alikuwa amemsihi hivi: “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, acha niende kisirisiri, ili niwaone ndugu zangu.” Yonathani hakuogopa kusema kwamba Daudi alipata kibali chake. Mfalme alikasirika sana! Alimtukana Yonathani na kufoka kwamba Daudi angemzuia mwanawe asiwe mfalme baada yake. Sauli alimwamuru Yonathani amlete Daudi kwake ili auawe. Yonathani akajibu hivi: “Kwa nini auawe? Amefanya nini?” Kwa hasira, Sauli akamrushia mkuki mwana wake. Yonathani aliponyoka bila jeraha lakini aliumizwa sana moyoni kuhusiana na Daudi.—1 Samweli 20:25-34.

      Yonathani alionyesha ushikamanifu kama nini! Kwa maoni ya wanadamu, urafiki wake na Daudi haungemfaidi sana, badala yake ungemletea hasara kubwa sana. Lakini, Yehova alikuwa ameagiza Daudi awe mfalme baada ya Sauli, na kusudi la Mungu lingemfaidi Yonathani na watu wengine pia.

      Kuagana kwa Machozi

      Yonathani alikutana na Daudi kisiri ili kumpasha habari. Ilikuwa wazi kwamba Daudi hangeweza tena kuingia kwenye makao ya Sauli. Wanaume hao wawili walilia na kukumbatiana. Kisha Daudi akakimbia mafichoni.—1 Samweli 20:35-42.

      Yonathani alikutana na mkimbizi huyo kwa mara ya mwisho, Daudi alipomkimbia Sauli na kujificha “katika nyika ya Zifu kule Horeshi.” Huo ndio wakati Yonathani alimtia moyo Daudi kwa maneno haya: “Usiogope; kwa kuwa mkono wa Sauli baba yangu hautakupata, na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli, na mimi nitakuwa wa pili kwako; na Sauli baba yangu pia anajua jambo hilo.” (1 Samweli 23:15-18) Muda mfupi baadaye, Yonathani na Sauli wakafa katika vita walipokuwa wakipigana na Wafilisti.—1 Samweli 31:1-4.

      Wote wanaompenda Mungu wanapaswa kutafakari mwenendo wa Yonathani. Je, unahitaji kuwa mshikamanifu kwa pande mbili tofauti? Ikiwa ndivyo, kumbuka kwamba Sauli alimhimiza Yonathani afuatie faida zake mwenyewe. Hata hivyo, Yonathani alimheshimu Yehova na akajitiisha kwake kutoka moyoni na kushangilia kwamba Mungu alikuwa amemchagua mfalme wa Israeli ambaye angefuata. Ndiyo, Yonathani alimuunga Daudi mkono, naye alikuwa mshikamanifu kwa Yehova.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki