Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika 1935, Frank Dewar, mwenyeji wa New Zealand, alisafiri pamoja na kikundi cha mapainia hao ndani ya Lightbearer mbali sana hadi Singapore. Kisha kabla tu ya mashua hiyo kusonga mbele hadi pwani ya kaskazini-magharibi mwa Maleya, Kapteni Eric Ewins akasema: “Basi, Frank, tumefika. Hapa ndipo tuwezapo kukufikisha. Ulichagua kwenda Siam. Basi, shuka ushike njia!” Lakini Frank alikuwa karibu amesahau habari za Siam. Alikuwa akifurahia utumishi pamoja na kikundi hicho ndani ya mashua. Sasa alikuwa peke yake.

      Alitua katika Kuala Lumpur mpaka aweze kuchuma pesa za kutosha kuendelea na safari, lakini, alipokuwa huko, alipatwa na aksidenti ya gari—lori lilimgonga na kumwangusha kutoka baiskeli yake. Baada ya kupata nafuu, akiwa na dola tano tu katika mfuko wake, alipanda garimoshi lililokuwa likisafiri kutoka Singapore hadi Bangkok. Lakini akiwa na imani katika uwezo wa Yehova wa kuruzuku, akaanza kazi. Claude Goodman alikuwa amehubiri huko kifupi katika 1931; lakini wakati Frank alipowasili katika Julai 1936, hakukuwa na Mashahidi wa kumlaki.

  • Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 447]

      Frank Dewar (anayeonyeshwa hapa akiwa na mke wake na mabinti wao wawili) alienda Thailand katika 1936 akiwa painia peke yake na alikuwa angali painia wa pekee katika 1992

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki