-
Visababishi na Hatari za JongoAmkeni!—2012 | Agosti
-
-
Kunenepa kupita kiasi na aina ya vyakula: Kitabu Encyclopedia of Human Nutrition kinasema hivi: “Siku hizi ugonjwa wa jongo haudhibitiwi hasa kwa kuepuka tu vyakula vilivyo na purini nyingi, bali pia kwa kutibu matatizo ya umeng’enyaji yanayohusianishwa na jongo kama vile: kunenepa kupita kiasi, tatizo la kukosa kutokeza insulini, na dyslipidemia,” au kuweko kwa viwango vya juu vya shahamu kwenye damu, kama vile kolesteroli.
Hata hivyo, wataalamu fulani hupendekeza kupunguza vyakula vyenye purini nyingi kama vile, hamira, aina fulani ya samaki, na aina mbalimbali za nyama nyekundu.b
Kileo: Kutumia kileo kupita kiasi kunaweza kufanya iwe vigumu kwa mwili wako kuondoa asidi ya yurea, na hivyo kuifanya irundamane.
-
-
Visababishi na Hatari za JongoAmkeni!—2012 | Agosti
-
-
Mambo Matano Yanayoweza Kuzuia Jongo Isitokee Tena
Kwa sababu jongo imehusianishwa na mtindo wa maisha, madokezo yafuatayo huenda yakawasaidia watu kupunguza uwezekano wa jongo kutokea tena.c
1. Kwa sababu jongo ni ugonjwa unaotokea mwili unaposhindwa kumeng’enya madini, wagonjwa wanapaswa kujitahidi kudumisha uzito unaofaa kwa kupunguza kiasi cha kalori wanachokula. Isitoshe, kunenepa kupita kiasi kunaongeza uzito kwenye vifundo.
2. Jihadhari na mbinu za kupunguza uzito kwa ghafla, ambazo zinaweza kuongeza kiasi cha asidi ya yurea katika damu.
3. Epuka kula kiasi kikubwa cha protini inayotokana na wanyama. Watu fulani hupendekeza mtu ale gramu 170 hivi kila siku za nyama isiyo na mafuta mengi, kama vile nyama ya kuku na samaki.
4. Ikiwa wewe hunywa kileo, fanya hivyo kwa kiasi. Unapopatwa na jongo, huenda likawa jambo la busara kuepuka kabisa kunywa kileo.
5. Kunywa kiasi kikubwa cha vinywaji visivyo na kileo. Hilo linasaidia kuyeyusha na kuondoa asidi ya yurea mwilini.d
Hatua za kuzuia jongo zilizotajwa hapo juu huenda zikatukumbusha amri ya Biblia kwamba tuwe wenye “kiasi katika mazoea” na tusinywe “divai nyingi.” (1 Timotheo 3:2, 8, 11) Kwa hakika Muumba wetu mwenye upendo anajua mambo yanayotufaa.
-
-
Visababishi na Hatari za JongoAmkeni!—2012 | Agosti
-
-
b Kulingana na makala iliyochapishwa katika jarida Australian Doctor, “hakuna uthibitisho unaoonyesha kuwa mtu anaweza kupatwa na ugonjwa wa jongo” kwa kula uyoga na mboga zilizo na purini nyingi, kama vile maharagwe, dengu, njegere, spinachi, na koliflawa.
-