Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Lazima Tuote Ndoto
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • Watu fulani huhisi kwamba habari za ndoto zao zina ujumbe wa pekee kwa ajili yao. Ili ndoto zifafanuliwe, wao huweka kitabu cha kuandikia karibu na kitanda chao ili waweze kuzirekodi wanapoamka. Kuhusiana na faida ya vitabu vinavyojaribu kutoa maana ya mifano ya ndoto, The Dream Game, kilichoandikwa na Ann Faraday, chasema: “Vitabu vya ndoto ambavyo katika hivyo unachunguza maana ya vichwa na mifano ya ndoto havina faida vilevile, viwe ni vya kimapokeo au vinategemea nadharia fulani ya kisaikolojia ya kisasa.”

      Kwa kuwa yaonekana kwamba ndoto hutokea katika ubongo hasa, haifai kufikiri kwamba zina ujumbe mbalimbali wa pekee kwa ajili yetu. Twapaswa kuziona kuwa utendaji wa kawaida wa ubongo unaosaidia kuudumisha ukiwa wenye afya.

  • Je, Ndoto Zaweza Kutabiri Wakati Ujao?
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • TANGU nyakati za kale, wanadamu wamekuwa na upendezi mwingi katika ndoto. Wamisri walitayarisha vitabu vyenye maelezo mengi vya kufafanua ndoto, na Wababiloni walikuwa na wafafanuzi wao wa ndoto. Miongoni mwa Wagiriki desturi ilikuwa kuwafanya wagonjwa walale katika mahekalu ya Asclepius ili kupata maagizo juu ya afya katika ndoto zao. Katika karne ya pili ya Wakati wa Kawaida wetu, Artemidorus alitokeza kitabu ambacho katika hicho alitoa ufafanuzi wa mifano ya ndoto. Vitabu vingi vinavyofanana na hicho ambavyo vimetokezwa tangu wakati ule vimetegemea kitabu chake. Kufikia leo, jitihada zinafanywa ili kufafanua ndoto, lakini je, kweli zinatoa ufahamu wenye kina katika matukio ya wakati ujao?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki