-
Mungu Aanza Kuumba VituKitabu Changu cha Hadithi za Biblia
-
-
HADITHI YA 1
Mungu Aanza Kuumba Vitu
VITU vizuri vyote tulivyo navyo vimetoka kwa Mungu. Aliumba jua litupe mwangaza mchana, mwezi na nyota usiku. Tena Mungu akaumba dunia tukae ndani yake.
Lakini kwanza Mungu hakuumba jua, mwezi, nyota na dunia. Unajua alivyoumba kwanza? Mungu aliumba watu walio kama yeye. Hatuwezi kuona watu hao, kama vile hatuwezi kumwona Mungu. Biblia inawaita watu hao malaika. Mungu aliumba malaika wakae na yeye mbinguni.
Malaika ambaye Mungu aliumba kwanza alikuwa wa pekee sana. Alikuwa Mwana wa kwanza wa Mungu, akafanya kazi pamoja na Baba yake. Alimsaidia Mungu kuumba vitu vingine vyote. Tena alimsaidia Mungu kuumba jua, mwezi, nyota na dunia yetu.
Wakati huo dunia ilikuwa namna gani? Mwanzoni mtu hangeweza kukaa duniani. Nchi yote ilikuwa bahari kubwa. Lakini Mungu alitaka watu wakae duniani. Akaanza kutayarisha makao yetu. Alifanya nini?
Kwanza dunia ilitaka nuru. Basi Mungu akaifanya nuru ya jua iangazie dunia. Alifanya hivyo ili kuwe usiku na mchana. Kisha Mungu akatokeza nchi kavu juu ya maji ya bahari.
Kwanza nchi haikuwa na kitu. Ilikuwa kama picha unayoona hapa. Maua hayakuwapo, wala miti wala wanyama. Hata samaki hawakuwamo baharini. Mungu alikuwa na kazi zaidi ili dunia iwe makao yanayofaa sana ya wanyama na watu.
-
-
Bustani NzuriKitabu Changu cha Hadithi za Biblia
-
-
HADITHI YA 2
Bustani Nzuri
TAZAMA dunia hii! Kila kitu ni kizuri sana! Tazama majani na miti, maua na wanyama wote. Unaweza kumjua tembo na simba hapa?
Bustani hii nzuri ilitokea namna gani? Na tuone Mungu alivyotuwekea dunia tayari.
Kwanza, Mungu aliumba majani mabichi yaifunike nchi. Alifanya namna zote za mimea na miti midogo. Mimea hiyo inapamba dunia. Zaidi ya hivyo, mimea mingi inatupa chakula kitamu sana.
Tena Mungu aliumba samaki waogelee katika maji na ndege waruke katika anga. Aliumba mbwa na paka na farasi; wanyama wakubwa na wadogo. Ni wanyama gani wanaokaa karibu na nyumba yenu? Je! si vizuri kufurahi kwa vile Mungu alitufanyia vyote hivyo?
Halafu, Mungu alifanya sehemu moja ya dunia kuwa ya pekee sana. Aliita bustani ya Edeni. Ilikuwa nzuri sana. Kila kitu ndani kilikuwa kizuri. Mungu alitaka dunia nzima iwe kama bustani nzuri hii.
Lakini tazama tena picha hii ya bustani. Je! unajua kitu ambacho Mungu aliona hakipo? Tuone.
-