-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Mabaki Wayahudi waliorudishwa ndio waliokuwa “dunia mpya,” yaani jamii iliyosafishwa, nao walijitiisha chini ya utawala huo na kusaidia kuanzisha upya ibada safi nchini. (Ezra 5:1, 2)
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
22. Dunia mpya itafanyizwa kwa watu gani, na watu wanatayarishwaje hata sasa ili wawe kiini cha mpango huo?
22 Namna gani dunia mpya? Kwa kufuata kielelezo cha utimizo wa kale, dunia mpya itafanyizwa kwa watu wanaofurahia kujitiisha chini ya utawala wa serikali mpya ya kimbingu. Hata sasa, mamilioni ya watu mmoja-mmoja wenye mwelekeo unaofaa wananyenyekea chini ya serikali hiyo na kujitahidi kufuata sheria zake zilizo katika Biblia. Wanatoka katika taifa zote, lugha zote, na jamii zote, nao hushirikiana kumtumikia Mfalme Yesu Kristo anayetawala. (Mika 4:1-4) Mfumo mwovu wa mambo uliopo ukiisha kupita, kikundi hicho ndicho kitakachofanyizwa kuwa kiini cha dunia mpya na hatimaye kiwe jamii ya wanadamu wenye kumhofu Mungu watakaokuwa kila mahali ulimwenguni, wakiwa warithi wa makao ya kidunia ya Ufalme wa Mungu.—Mathayo 25:34.
-
-
‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kupitia Isaya, Yehova anasema hivi: “Tazama, mimi ninaumba mbingu mpya na dunia mpya, na maneno ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.” (Isaya 65:17, “Zaire Swahili Bible”)
-