-
Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
-
-
Sababu ya tatu ya sisi kuhitaji chakula, lasema gazeti Food and Nutrition, ni “kurekebisha afya ya mwili. . . na kuzuia maradhi.” Manufaa za kiafya za chakula kizuri hazionekani wazi mara moja. Tumalizapo mlo mzuri, ni mara chache tufikiriapo, ‘Mlo huo umenufaisha sana moyo wangu (au mafigo yangu au misuli yangu, na kadhalika).’ Hata hivyo, jaribu kutokula kwa kipindi fulani, na matokeo kwa afya yako yataonekana wazi. Matokeo gani? “Tokeo lililo la kawaida zaidi,” chasema kitabu cha marejezo ya kitiba, “ni lenye kudhuru: kushindwa kukua, kushindwa kukinza maambukizo madogo-madogo, ukosefu wa nishati au uanzisho.”
-
-
Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
-
-
“Mlo mzuri ndio uhitaji wa msingi zaidi wa binadamu. . . . Bila chakula cha kutosha, tungekufa.”—Food and Nutrition.
KWELI hiyo ya msingi inatolewa kielezi vizuri na miili iliyodhoofika kwa njaa ya wanaume, wanawake, na watoto wanaonyimwa “uhitaji [huu ulio] wa msingi zaidi wa binadamu.” Wengine wanaweza kukabili uhitaji huo kwa kadiri fulani lakini bado wana ukosefu mkubwa wa lishe bora. Hata hivyo, wengi ambao wangeweza kula vizuri mara nyingi huridhika na chakula kisichojenga mwili ambacho huandaa lishe ndogo kihalisi. “Chakula,” lasema gazeti Healthy Eating, “chaonekana kuwa mojawapo ya mali zetu zenye kutumiwa vibaya zaidi.”
-