Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuunganisha Ulimwengu-Mazuri na Mabaya Yanayotarajiwa
    Amkeni!—2002 | Mei 22
    • Wachanganuzi fulani wanaona faida nyingine ya kuunganisha uchumi wa ulimwengu: Wanaonelea kwamba jambo hilo litazuia mataifa kushiriki katika vita. Katika kitabu chake kinachoitwa The Lexus and the Olive Tree, Thomas L. Friedman anasema kwamba utandaridhi ‘unawachochea watu sana wasipigane na kuongeza gharama za vita sana kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya kisasa.’

  • Kuunganisha Ulimwengu-Mazuri na Mabaya Yanayotarajiwa
    Amkeni!—2002 | Mei 22
    • Kuhofu Kwamba Ulimwengu Utagawanyika Zaidi

      Huenda hangaiko kuu kuhusu utandaridhi ni jinsi ambavyo umezidisha ile tofauti kati ya matajiri na maskini. Ijapokuwa ni wazi kwamba utajiri wa ulimwengu umeongezeka, ni watu wachache zaidi na nchi chache zaidi zilizo na utajiri huo. Sasa mali halisi za watu 200 matajiri zaidi ulimwenguni ni nyingi kuliko jumla ya mapato ya watu bilioni 2.4 hivi wanaoishi duniani—asilimia 40 ya watu wote duniani. Na ijapokuwa mapato yanaendelea kuongezeka katika nchi tajiri, mapato ya wastani katika nchi 80 zenye umaskini yamepungua katika muda wa miaka kumi iliyopita.

      Hangaiko jingine la maana linahusu mazingira. Utandaridhi wa kiuchumi umechochewa na shughuli za biashara zinazokazia faida za kiuchumi kuliko kuhifadhi mazingira. Agus Purnomo, msimamizi wa Hazina ya Mazingira ya Ulimwenguni Pote huko Indonesia, anaeleza tatizo hilo hivi: ‘Tunataka maendeleo daima. Nina wasiwasi kwamba baada ya miaka kumi, tutakuwa tumefahamu umuhimu wa kutunza mazingira, lakini hakutakuwa na viumbe wa kuhifadhi.’

      Watu pia wanahangaikia kazi zao. Imekuwa rahisi zaidi kupoteza kazi na mapato kwa sababu mashirika yanayoungana ulimwenguni pote na mashindano makali katika biashara yanalazimu makampuni kuboresha huduma zao. Makampuni yanayohangaikia kupata faida kubwa huona kwamba ni jambo la busara kuwaajiri na kuwafuta wafanyakazi kwa kutegemea faida inayopatikana, lakini jambo hilo huwaletea watu matatizo makubwa.

      Kuongezeka kwa mikopo na fedha za kigeni ulimwenguni pote kumetokeza tatizo jingine. Watega-uchumi wa kimataifa wanaweza kukopesha nchi zinazoendelea fedha nyingi sana lakini baadaye kuondoa fedha zao kwa ghafula wakati hali ya uchumi inapozorota. Wakati fedha hizo zinapoondolewa nchi zinazohusika zinaweza kukumbwa na matatizo ya kiuchumi. Mnamo mwaka wa 1998, watu milioni 13 walifutwa kazi huko Asia Mashariki kwa sababu ya hali mbaya za kiuchumi. Huko Indonesia, mapato halisi ya wale wafanyakazi ambao hawakufutwa kazi yalipungua kwa asilimia 50.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki