Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wamishonari Wasukuma Mpanuko wa Ulimwenguni Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika miji iliyo karibu Ibarra, Ekuado, Unn Raunholm na Julia Parsons walikabili tena na tena magenge yaliyochochewa na mapadri. Kwa sababu padri alifanyiza ghasia kila wakati wamishonari walipoenda San Antonio, dada waliamua kukazia fikira mji mwingine, uitwao Atuntaqui. Lakini siku moja mkuu wa eneo hilo akiwa mwenye wasiwasi alimhimiza Dada Raunholm aondoke mji huo upesi. “Padri anapanga maandamano dhidi yako, na sina watu wa kutosha kukulinda,” akajulisha. Yeye akumbuka waziwazi: “Umati ulikuwa unatujia! Ile beramu nyeupe na ya manjano ya Vatikani ilipeperushwa mbele ya kikundi hicho huku padri akipaza sauti shime kama vile ‘Kanisa Katoliki na lidumu daima!’ ‘Waprotestanti na watokomee mbali!’ ‘Ubikira wa Bikira na uendelee daima!’ ‘Maungamo na yaendelee daima!’ Kila wakati, umati ungerudia shime hizo neno kwa neno baada ya padri.” Wakati uo huo, wanaume kadhaa wakawaalika Mashahidi hao ndani ya Nyumba ya Wafanyakazi ili wapate usalama. Humo, wamishonari hao walijishughulisha kutoa ushahidi kwa watu wenye udadisi waliokuja kuona kile kilichokuwa kikiendelea. Waliangusha fasihi zote walizokuwa nazo.

  • Wamishonari Wasukuma Mpanuko wa Ulimwenguni Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 543]

      Unn Raunholm, mishonari tangu 1958, alilazimika kukabili magenge yaliyoongozwa na mapadri katika Ekuado

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki