-
Majitu Yalipokuwa Yamejaa UlayaAmkeni!—2009 | Mei
-
-
Majitu Yalipokuwa Yamejaa Ulaya
NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI ITALIA
MNAMO 1932, wajenzi wa barabara walikuwa wakichimba karibu na uwanja wa Colosseum huko Rome wakati mmoja wao alipogonga kitu fulani kigumu. Kumbe kilikuwa ni pembe na fuvu la tembo. Huo haukuwa ugunduzi wa pekee. Kwa miaka mingi, mabaki ya tembo 140 yamepatikana huko Rome na katika maeneo ya karibu. Mabaki ya kwanza yalipatikana katika karne ya 17.
-
-
Majitu Yalipokuwa Yamejaa UlayaAmkeni!—2009 | Mei
-
-
Mabaki au visikuku vya tembo vilivyochimbuliwa huko Italia havifanani na ya tembo wa leo. Badala yake, mabaki hayo ni ya jamii ya tembo iliyotoweka inayoitwa Elephas antiquus, au tembo wa kale. (Ona ukurasa wa 15.) Tembo huyo alikuwa na pembe zilizonyooka na alikua kufikia kimo cha mita 5 kwenye mabega, kimo kinachozidi tembo wa leo kwa mita 2 hivi.
Majitu hayo yalikuwa mengi kadiri gani? Rekodi ya vitu vya kale vilivyochimbuliwa inaonyesha kwamba wakati mmoja tembo hao walipatikana katika sehemu zote za Ulaya na Uingereza, kama tu tembo wengine wa jamii yao wanaoitwa mammoth.
-