-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Kwa kufaa, hao mashahidi wawili wanaonwa sasa wakifanya ishara zinazokumbusha zile za Musa na Eliya. Mathalani, Yohana anasema hivi kwa habari yao: “Na ikiwa yeyote anataka kudhuru wao, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao; na ikiwa yeyote angepaswa kutaka kudhuru wao, kwa jinsi hii yeye lazima auawe. Hawa wana mamlaka kufunga mbingu ili kwamba mvua isianguke wakati wa kutoa kwao unabii.”—Ufunuo 11:5, 6a, NW.
-
-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
17. (a) Ni matukio gani katika siku za Eliya yaliyohusu ukame na moto? (b) Moto ulitokaje katika vinywa vya mashahidi wawili, na ni ukame gani uliohusika?
17 Vipi Eliya? Katika siku za wafalme wa Israeli, nabii huyu alipiga mbiu ya ukame kuwa wonyesho wa ghadhabu ya Yehova juu ya Waisraeli waabudu-Baali. Uliendelea kwa miaka mitatu na nusu. (1 Wafalme 17:1; 18:41-45; Luka 4:25; Yakobo 5:17) Baadaye, wakati Mfalme Ahazi alipotuma askari-jeshi wamlazimishe Eliya aje ndani ya kuwapo kwake kwa kifalme, nabii huyo aliita moto kutoka mbinguni uteketeze askari-jeshi hao. Ni wakati tu kamanda wa kivita alipoonyesha heshima inayofaa cheo chake akiwa nabii ndipo Eliya alikubali kuandamana naye kwenda kwa mfalme. (2 Wafalme 1:5-16) Hali kadhalika, kati ya 1914 na 1918, baki la wapakwa-mafuta lilivuta uangalifu kwa ujasiri kwenye hali ya ukame wa kiroho katika Jumuiya ya Wakristo na likaonya juu ya hukumu yenye moto kwenye “ile siku kubwa na yenye kuvuvia hofu ya Yehova inayokuja.”—Malaki 4:1, 5; Amosi 8:11, NW.
-