-
Kukumbwa na Mfadhaiko!Amkeni!—2005 | Februari 8
-
-
Kulingana na shirika moja la Marekani, “kisababishi kikuu cha mfadhaiko miongoni mwa watu wazima ni kazi (asilimia 39), na kisababishi cha pili ni familia (asilimia 30). Visababishi vingine vya mfadhaiko vinatia ndani afya (asilimia 10), mahangaiko kuhusu uchumi (asilimia 9), na mahangaiko kuhusu mizozo ya kimataifa na ugaidi (asilimia 4).”
Mfadhaiko haulemei Marekani tu. Katika uchunguzi uliofanywa huko Uingereza mwaka wa 2002, ilikadiriwa kwamba “katika mwaka wa 2001 na 2002, zaidi ya watu nusu milioni nchini Uingereza walifadhaishwa sana na kazi kiasi cha kuwa wagonjwa.” Inakadiriwa kwamba “siku za kazi milioni kumi na tatu na nusu hupotea kila mwaka nchini Uingereza” kwa sababu ya “mfadhaiko unaosababishwa na kazi, kushuka moyo, au mahangaiko.”
Nchi nyingine za Ulaya zinakumbwa pia na hali hiyo. Kulingana na Shirika la Ulaya la Usalama na Afya Kazini, “mamilioni ya watu wanaofanya kazi tofauti-tofauti huko Ulaya wamefadhaishwa na kazi.” Uchunguzi mmoja ulionyesha kwamba “kila mwaka wafanyakazi milioni 41 hivi [katika Muungano wa Ulaya] hufadhaishwa na kazi.”
Vipi juu ya Asia? Ripoti moja iliyotolewa na kongamano lililofanywa huko Tokyo inasema: “Mfadhaiko unaosababishwa na kazi huathiri sana nchi nyingi ulimwenguni, ziwe ni nchi zinazoendelea au zilizoendelea.” Ripoti hiyo ilisema kwamba “nchi kadhaa katika Asia Mashariki, kama vile China, Korea na Taiwan, zimesitawi haraka kiviwanda na kiuchumi. Sasa nchi hizo zinahangaikia sana mfadhaiko unaosababishwa na kazi na jinsi unavyoathiri sana afya ya wafanyakazi.”
-
-
Visababishi na Madhara ya MfadhaikoAmkeni!—2005 | Februari 8
-
-
Ripoti ya Shirika la Ulaya la Usalama na Afya Kazini inasema kwamba mara nyingi wafanyakazi hukumbwa na mfadhaiko wanapokuwa kazini kwa sababu mbalimbali kama vile, mawasiliano yasiyofaa baina yao na wasimamizi, kukosa uhuru wa kutosha wa kufanya maamuzi yanayowahusu, kukosana na wafanyakazi wenzao, uwezekano wa kufutwa kazi au kwa sababu ya kulipwa mshahara mdogo. Hata sababu iwe nini, kushughulika na mfadhaiko unaosababishwa na kazi kunaweza kuwafanya wazazi washindwe kushughulikia mahitaji ya familia zao. Familia zinaweza kuwa na mahitaji mengi.
-