Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ulaya Iliyoungana—Kwa Nini Ni Jambo Linalopasa Kufikiriwa?
    Amkeni!—2000 | Aprili 22
    • VIZIBO vya shampeni viliruka kwa kelele. Fataki zikaangaza anga. Ni nini kilichokuwa kikisherehekewa? Je, ni milenia mpya? La, kwa wazi tukio hili lilikuwa la maana zaidi ya kubadili kalenda kutoka mwaka wa 1999 hadi mwaka wa 2000. Ilikuwa Januari 1, 1999. Fedha mpya ya pamoja ya Muungano wa Ulaya (EU)—fedha inayoitwa euro—ilikuwa imeanzishwa rasmi siku hiyo.

      Wazungu wengi wanaona kuanzishwa kwa fedha ya pamoja kuwa hatua ya kihistoria katika jitihada ya muda mrefu ya kuunganisha Ulaya. Gazeti la Uholanzi la De Telegraaf lilisifu kuanzishwa kwa euro kuwa “heshima ya kuunganishwa kwa Ulaya.” Kwa kweli, baada ya miongo mingi ya mradi uliotamaniwa, diplomasia, na kuchelewa, sasa muungano wa Ulaya waelekea kufikiwa kuliko wakati mwingine wowote.

      Ni kweli kwamba watu wasioishi Ulaya huenda wakajiuliza ni nini hiki kinachowasisimua watu. Kuanzishwa kwa euro na jitihada za kuunganisha Ulaya huenda zisiathiri kwa vyovyote maisha yao ya kila siku. Hata hivyo, kuunganishwa kwa Ulaya kungetokeza mojawapo ya jumuiya zenye uwezo mkubwa zaidi wa kiuchumi ulimwenguni. Kwa hiyo bila kujali unaishi wapi—hungekosa kutambua Ulaya iliyoungana.

      Kwa mfano, hivi karibuni Waziri Msaidizi wa Mashauri ya Nchi za Kigeni wa Marekani Marc Grossman aliwaambia hivi wasikilizaji wa Amerika Kaskazini: “Ufanisi wetu unahusiana na Ulaya.” Kwa nini? Baadhi ya sababu alizotaja ni kwamba “1 kati ya wafanyakazi wa viwandani 12 wa Marekani, hufanya kazi katika mojawapo ya viwanda 4,000 vinavyomilikiwa na Wanaulaya huko Marekani.” Pia inaripotiwa kwamba huenda fedha mpya ya Ulaya ikaathiri bei za bidhaa zinazoingizwa nchini—na hata viwango vya rehani—katika nchi zilizo mbali na Ulaya.

      Huenda nchi zinazositawi zikanufaika. Jinsi gani? Uchunguzi mmoja wasema hivi: “Kuondolewa kwa fedha mbalimbali za Ulaya na kuwepo kwa euro kutarahisisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi zinazositawi na EU.” Kwa kuongezea, watu fulani wanatabiri kwamba mashirika ya biashara ya Japani na Marekani yanayofanya biashara Ulaya yatanufaika. Baada ya euro kuimarika, hakutakuwa na kubadilika-badilika kwa viwango vya ubadilishaji wa fedha kati ya nchi za Ulaya. Huenda kukawa na faida kubwa kufanya biashara Ulaya.

      Ikiwa unapanga kusafiri Ulaya, huenda vilevile ukaona manufaa ya kuunganishwa kwa Ulaya. Karibuni utaweza kununua bidhaa katika nchi tofauti-tofauti za Ulaya kwa kutumia fedha ileile, euro, ambayo thamani yake inakaribia dola ya Marekani. Watalii hawatatatanika tena kushughulika na gulden, faranga, lira, maki, na mashine za mfukoni za kupigia hesabu.

  • Ulaya Iliyoungana—Kwa Nini Ni Jambo Linalopasa Kufikiriwa?
    Amkeni!—2000 | Aprili 22
    • [Picha katika ukurasa wa 1]

      Euro itachukua mahali pa fedha nyingi za Ulaya

      [Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

      Euro na ishara za euro kwenye ukurasa wa 3, 5-6, na 8: © European Monetary Institute

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki