-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Kupeleka Kweli Zenye Thamani Kwenye Nchi za Kwao
Tamaa yenye kuwaka ya kushiriki kweli muhimu za Biblia ilihimiza watu wengi warudi kwenye nchi zao walimozaliwa ili kushiriki katika kazi ya kueneza evanjeli. Itikio lao lilikuwa kama lile la watu wa kutoka nchi nyingi waliokuwa katika Yerusalemu katika 33 W.K. na ambao walipata kuwa waamini wakati roho takatifu iliposukuma mitume na washiriki wao waseme kwa lugha nyingi, kuhusu “mambo yenye fahari ya Mungu.” (Mdo. 2:1-11, NW) Kama vile tu waamini hao wa karne ya kwanza walivyopeleka kweli kwenye nchi zao, ndivyo na hawa wanafunzi wa kisasa.
Wanaume kwa wanawake waliokuwa wamejifunza kweli ng’ambo walirudi Italia. Walitoka Amerika, Ubelgiji, na Ufaransa wakatangaza kwa bidii ujumbe wa Ufalme mahali walipokaa. Makolpota kutoka mkoa wa Tisino wa Uswisi wenye kusema Kiitalia walihamia Italia pia waendelee na kazi yao. Ingawa idadi yao ilikuwa ndogo, kama tokeo la utendaji wao wa umoja, upesi walifikia karibu kila jiji kuu na vingi vya vijiji vya Italia. Wao hawakuwa wakihesabu saa walizotumia katika kazi hiyo. Wakisadiki kwamba walikuwa wakihubiri kweli ambazo Mungu alitaka watu wazijue, mara nyingi walifanya kazi tokea asubuhi hadi usiku ili kufikia watu wengi iwezekanavyo.
Wagiriki waliokuwa wamekuwa Wanafunzi wa Biblia katika Albania ya karibu na mbali kama vile Amerika pia walielekeza fikira kwenye nchi ya kwao. Walisisimuka kujifunza kwamba ibada ya sanamu si ya Kimaandiko (Kut. 20:4, 5; 1 Yoh. 5:21), kwamba watenda dhambi hawachomwi katika moto wa helo (Mhu. 9:5, 10; Eze. 18:4; Ufu. 21:8), na kwamba Ufalme wa Mungu ndio tumaini pekee la kweli kwa wanadamu (Dan. 2:44; Mt. 6:9, 10). Walikuwa na hamu ya kushiriki kweli hizo pamoja na wananchi wenzao—kibinafsi au kwa barua. Kama tokeo, vikundi vya Mashahidi wa Yehova vikaanza kusitawi katika Ugiriki na visiwa vya Ugiriki.
Kufuatia Vita ya Ulimwengu 1, maelfu ya watu kutoka Poland walihamia Ufaransa ili kufanya kazi ya kuchimba makaa-mawe. Makutaniko ya Kifaransa hayakuwapuuza kwa sababu walisema lugha tofauti. Walipata njia za kushiriki kweli za Biblia pamoja na wachimbaji hao na familia zao, na idadi ya walioitikia vizuri ikazidi upesi ile ya Mashahidi Wafaransa. Wakati serikali ilipotoa amri ya kuwarudisha kwao, 280 walilazimika kurudi Poland katika 1935, hiyo ilitumika tu kuimarisha kazi ya kueneza ujumbe wa Ufalme huko. Hivyo, katika 1935, kulikuwa wapiga-mbiu wa Ufalme 1,090 walioshiriki kutoa ushahidi nchini Poland.
-
-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Ramani katika ukurasa wa 428]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Wakati wahamaji kutoka nchi zilizotajwa katika ramani hii walipojifunza juu ya kusudi la ajabu la Mungu la kubariki wanadamu, walihisi wakilazimika kurudi wapeleke habari hiyo katika nchi za kwao
MABARA YA AMERIKA
↓ ↓
AUSTRIA
BULGARIA
SAIPRASI
CHEKO-SLOVAKIA
DENMARK
FINLAND
UJERUMANI
UGIRIKI
HUNGARIA
ITALIA
UHOLANZI
NORWAY
POLAND
URENO
RUMANIA
HISPANIA
SWEDEN
USWISI
UTURUKI
YUGOSLAVIA
-