-
Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Pia alisafiri Ulaya katika 1891 ili kuona ni jambo gani lingeweza kufanywa ili kusogeza mbele kuenezwa kwa kweli huko. Safari hiyo ilimpeleka Ireland, Scotland, Uingereza, nyingi za nchi za bara la Ulaya, Urusi (lile eneo liitwalo sasa Moldova), na Mashariki ya Kati.
Alifikia mkataa gani baada ya kuwasiliana na watu katika safari hiyo? “Sisi hatukuona kufunguka au utayari kwa ajili ya kweli katika Urusi . . . Hatukuona jambo lolote la kututia moyo tutumainie vuno lolote katika Italia au Uturuki au Austria au Ujerumani,” akaripoti. “Lakini Norway, Sweden, Denmark, Uswisi, na hasa Uingereza, Ireland, na Scotland, ni mashamba yaliyo tayari na yanangojea kuvunwa. Mashamba hayo yaonekana yakilia, Njooni huku mtusaidie!”
-
-
Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Wakati Ndugu Russell alipotembelea Uingereza tena katika 1903, watu elfu moja walikusanyika katika Glasgow ili kumsikia akihutubu juu ya “Matumaini na Matarajio ya Mileani,” 800 walihudhuria katika London, na wasikilizaji 500 kufikia 600 katika miji mingine.
-
-
Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Kwa habari ya Austria, Ndugu Russell mwenyewe alirudi katika 1911 ili kutoa hotuba katika Vienna, ikawa tu kwamba mkutano ulikatizwa na wafanyaghasia.
-