-
UumbajiKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Katika ulimwengu huu wa kisasa, wa kisayansi, je, ni jambo linalopatana na akili kuamini uumbaji?
“Sheria za asili za ulimwengu ni sahihi sana hivi kwamba si vigumu kutengeneza vyombo vya angani viruke mpaka mwezini na tunaweza kupima kwa usahihi safari yake hata kwa sehemu ya sekunde. Lazima sheria hizo ziliwekwa na mtu fulani.”—Akasema Wernher von Braun, aliyehusika sana katika kuwatuma wanaanga wa Marekani mwezini.
-
-
UumbajiKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Robert White, daktari anayepasua ubongo, alisema: “Sina la kusema ila kukubali kwamba kuna Akili Iliyo Kubwa Zaidi, iliyobuni na kusitawisha uhusiano wa ajabu kati ya akili na ubongo—jambo ambalo mwanadamu hawezi kabisa kulielewa.” (The Reader’s Digest, Septemba 1978, uku. 99)
-