-
Tumia Vizuri Udadisi WakoMnara wa Mlinzi—2008 | Juni 1
-
-
Mfano Unaochochea
Bila shaka, udadisi una faida zake. Fikiria kisa cha Mjerumani Alexander von Humboldt, mtaalamu wa vitu vya asili na mvumbuzi aliyeishi katika karne ya 19 ambaye Mto Humboldt huko Amerika Kusini uliitwa jina lake.
Pindi moja maishani mwake, Humboldt alisema: “Tangu ujana wangu nilitamani sana kutembelea maeneo ya mbali, ambayo watu wa Ulaya waliyatembelea mara chache sana.” Anasema kwamba tamaa ya kutembelea maeneo hayo ilianza alipohisi, “akili yake ikimchochea kwa njia zisizozuilika.” Akiwa na umri wa miaka 29, alienda Amerika ya Kati na ya Kusini katika safari yake ya uvumbuzi ya miaka mitano. Habari aliyokusanya aliiandika katika mabuku 30 ya rekodi ya matukio ya safari zake.
Mambo yote yalimvutia Humboldt, kutia ndani kiwango cha joto la bahari, samaki wanaoishi humo, hata mimea aliyoona. Alipanda milima, akavumbua mito, na kuabiri bahari. Utafiti wa Humboldt uliwekea msingi nyanja mbalimbali za sayansi ya kisasa. Yote hayo yalitokana na udadisi wake mwingi, na katika maisha yake yote aliendelea kuwa na tamaa isiyotoshelezwa ya kupata ujuzi. Mwandikaji Mmarekani, Ralph Waldo Emerson, alisema hivi kumhusu: “Humboldt alikuwa mmoja wa watu wa ajabu . . . wanaotokea mara kwa mara, kana kwamba wanataka kutuonyesha yale ambayo akili ya mwanadamu inaweza kufanya, nguvu na uwezo wake mbalimbali.”
-
-
Tumia Vizuri Udadisi WakoMnara wa Mlinzi—2008 | Juni 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 19]
Alexander von Humboldt
-