-
Ukombozi Kuingia Katika Ulimwengu Mpya MwadilifuMnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 1
-
-
Watumishi wa Mungu Washambuliwa
6, 7. Kwa nini watumishi wa Yehova wanaweza kuwa na uhakika washambuliwapo wakati wa “dhiki kubwa”?
6 Baada ya kuharibu dini isiyo ya kweli, matengenezo ya kisiasa yatageukia watumishi wa Yehova. Shetani, “Gogu, wa nchi ya Magogu” katika unabii, asema hivi: “Nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama.” Akidhani ya kuwa wao ni mawindo rahisi, awashambulia kwa “jeshi kuu . . . , kama wingu kuifunika nchi.” (Ezekieli 38:2, 10-16) Watu wa Yehova wanajua kwamba shambulio hilo halitafua dafu kwa sababu wanamtumaini Yehova.
7 Farao na majeshi yake walipohisi kwamba walikuwa wamewanasa watumishi wa Mungu kwenye Bahari Nyekundu, Yehova aliwakomboa watu wake kimuujiza na kuyaharibu majeshi ya Misri. (Kutoka 14:26-28) Wakati wa “dhiki kubwa,” mataifa yanapohisi kwamba yamewanasa watu wa Yehova, kwa mara nyingine tena awaokoa kimuujiza: “Katika siku hiyo . . . ghadhabu yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu. Kwa maana katika wivu wangu na katika moto wa ghadhabu yangu nimenena.” (Ezekieli 38:18, 19) Ndipo upeo wa “dhiki kubwa” utakapokaribia!
-
-
Ukombozi Kuingia Katika Ulimwengu Mpya MwadilifuMnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 1
-
-
10. Neno la Mungu hufafanuaje upeo wa “dhiki kubwa”?
10 Kisha Yehova atokeza pigo la kifo dhidi ya mfumo wa Shetani: “Nami nitamhukumu [Gogu] kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake . . . Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.” (Ezekieli 38:22, 23) Masalio yote ya mfumo wa Shetani yanaharibiwa. Jamii yote ya kibinadamu ya watu wenye kumpuuza Mungu inaangamizwa. Huo ndio upeo wa “dhiki kubwa,” Har–Magedoni.—Yeremia 25:31-33; 2 Wathesalonike 1:6-8; Ufunuo 16:14, 16; 19:11-21.
-