Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, ‘Wewe Walikuza Yerusalemu Zaidi ya Furaha Yako Iliyo Kuu’?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 15
    • 2. Ezra alikuwa nani, naye alibarikiwaje?

      2 Kwa kielelezo, fikiria kuhani Ezra. Hata kabla ya kurudi katika nchi yake ya nyumbani, alikuwa ameendeleza kwa bidii masilahi ya ibada safi huko Yerusalemu. (Ezra 7:6, 10) Ezra alibarikiwa sana kwa jambo hilo. Yehova Mungu aligusa moyo wa mfalme wa Uajemi ili ampe Ezra pendeleo la kuongoza kikundi kingine cha wahamishwa wenye kurudi Yerusalemu. Zaidi ya hayo, mfalme aliwapa mchango mkubwa wa dhahabu na fedha ili “kuipamba nyumba ya BWANA iliyoko Yerusalemu.”—Ezra 7:21-27.

  • Je, ‘Wewe Walikuza Yerusalemu Zaidi ya Furaha Yako Iliyo Kuu’?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 15
    • Baraka na Madaraka

      5. Wakazi wa Yuda walipata baraka zipi nyingi siku za Ezra?

      5 Kikundi cha wahamishwa wapatao 6,000 waliorudi na Ezra kilileta michango ya dhahabu na fedha kwa ajili ya hekalu la Yehova. Michango hiyo ilikuwa yenye thamani iliyo sawa na dola milioni 35 za kisasa. Dhahabu na fedha hiyo ilipita kwa mara zipatazo saba ile ambayo wahamishwa wa kwanza waliweza kuleta. Ni lazima wakazi wa Yerusalemu na Yuda wawe walimshukuru Yehova kama nini kwa kupokea utegemezo huo wa kibinadamu na wa vitu vya kimwili! Lakini kubarikiwa sana na Mungu huleta daraka pia.—Luka 12:48.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki