-
Baraka za Yehova HututajirishaMnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 15
-
-
10 Fikiria kielelezo cha Laurel, aliyeugua polio na ambaye aliishi ndani ya pafu la chuma (mashine iliyomsaidia kupumua) kwa miaka 37.a Licha ya hali zake ngumu sana, alimtumikia Mungu kwa bidii hadi kifo. Kwa miaka mingi, Yehova alimbariki sana Laurel. Kwa mfano, aliweza kusaidia watu 17 wapate ujuzi sahihi wa kweli ya Biblia, ingawa alilazimika kutumia mashine hiyo saa 24 kwa siku! Hali yake inatukumbusha maneno haya ya mtume Paulo: “Niwapo dhaifu, ndipo niwapo mwenye nguvu.” (2 Wakorintho 12:10) Naam, mafanikio yoyote tuwezayo kupata katika kuhubiri habari njema hayatokani na uwezo na nguvu zetu wenyewe bali hutokana na msaada wa Mungu kupitia roho takatifu, anayowapa wale wanaoendelea kusikiliza sauti yake.—Isaya 40:29-31.
-
-
Baraka za Yehova HututajirishaMnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 17]
Licha ya hali ngumu sana, Laurel Nisbet alimtumikia Mungu kwa bidii
-