Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matatizo ya Pekee ya Familia za Kambo
    Amkeni!—2012 | Aprili
    • UNACHOWEZA KUFANYA

      Usipuuze hisia zako ukidhani kwamba utaacha kukata tamaa. Badala yake, chunguza ni matarajio gani yasiyotimizwa yanayokufanya utamauke. Kisha chunguza ni kwa nini ulitarajia jambo hilo ili uelewe ni kwa nini unashikamana nalo. Mwishowe, jaribu kutafuta jambo linaloweza kutimizwa kwa sasa. Ona mifano ifuatayo:

      1. Tangu mwanzo, nitawapenda watoto wangu wa kambo, nao watanipenda.

      Kwa nini? Sikuzote nimetamani kuwa na familia changamfu yenye uhusiano wa karibu.

      Tarajio halisi: Baada ya muda, upendo wetu unaweza kukua. Jambo muhimu kwa sasa ni kwamba tujihisi tukiwa salama na tuheshimiane katika familia.

      2. Kila mtu katika familia mpya atazoea hali haraka.

      Kwa nini? Tuko tayari kuanza maisha mapya.

      Tarajio halisi: Familia za kambo huchukua kati ya miaka minne hadi saba kuimarika. Matatizo yetu ni ya kawaida.

      3. Hatutazozana kuhusu pesa.

      Kwa nini? Upendo utatusaidia tusibishanie mambo madogo.

      Tarajio halisi: Masuala ya kifedha yanayohusiana na ndoa zetu za awali ni mazito. Huenda isiwe rahisi kushirikiana katika matumizi ya pesa.

  • Matatizo ya Pekee ya Familia za Kambo
    Amkeni!—2012 | Aprili
    • UNACHOWEZA KUFANYA

      • Pendezwa na wengine na uwe na hisia-mwenzi badala ya kuhukumu. Kwa mfano:

      Mwana wako akisema, “Ninamkosa baba yangu,” kubaliana naye. Badala ya kusema, “Lakini baba yako wa kambo anakupenda na kukujali kuliko baba yako mzazi,” unaweza kumwambia: “Lazima iwe unapitia hali ngumu. Hebu nieleze, ni nini hasa kinachokufanya umkose baba yako?”

      Badala ya kumlaumu mwenzi wako mpya wa ndoa kwa kusema, “Ikiwa ungekuwa mzazi mzuri mwana wako angekuwa na adabu zaidi,” mweleze hisia zako. Unaweza kumwambia: “Tafadhali mkumbushe Luke awe akinisalimu anapokuja nyumbani. Hilo litanifanya nihisi vizuri.”

      • Jaribuni kufahamiana zaidi wakati mnapokula, wakati wa tafrija, na wakati wa ibada.

      • Muwe na mikutano ya familia kwa ukawaida, na kila mtu awepo. Mruhusu kila mtu katika familia aeleze maoni yake bila kumkatiza, akianza na mambo mazuri kuhusu familia mpya kisha aeleze mahangaiko yake. Mheshimiane hata mnapokosa kupatana, na uwaruhusu wote katika familia watoe mapendekezo ya jinsi mambo yanavyoweza kushughulikiwa.

  • Matatizo ya Pekee ya Familia za Kambo
    Amkeni!—2012 | Aprili
    • UNACHOWEZA KUFANYA

      • Tanguliza ndoa yako. (Mwanzo 2:24) Tenga wakati wa kuwa pamoja na mwenzi wako mpya, na uhakikishe kwamba watoto wako wanajua wazi fungu lake katika familia. Kwa mfano, baba anaweza kuwaambia watoto wake hivi kabla hajaoa tena: “Ninampenda Anna, naye atakuwa mke wangu. Najua kwamba mtamtendea kwa njia inayofaa.”

      • Tenga wakati wa kuwa pamoja na kila mmoja wa watoto wako. Kutenga wakati hususa kunaonyesha kwamba wao ni muhimu kwako na kutawahakikishia kwamba unawapenda.

      • Tenga wakati wa kuwa pamoja na kila mtoto wa kambo ili ujenge uhusiano mzuri naye bila mzazi halisi kuwa mpatanishi.

      • Waruhusu watoto wawe sehemu ya familia bila kuwatazamia wapuuze familia yao ya zamani. Usiwalazimishe watoto wa kambo wakuite “Baba” au “Mama.” Mwanzoni, huenda watoto wenye umri mkubwa wasijihisi huru kutumia maneno kama “familia” au “sisi” wanapozungumza kuhusu familia ya kambo.

      • Mpe kila mtoto kazi za kufanya nyumbani, mahali pa kuketi kwenye meza ya kulia, na sehemu yake nyumbani. Hilo linatia ndani watoto ambao huja nyumbani mara kwa mara.

      • Mnaweza kuhamia nyumba nyingine au mbadili mpangilio wa nyumba ya zamani ili washiriki wapya wasijihisi kuwa ni wageni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki