Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Akina Baba Wanawezaje Kuwa na Uhusiano wa Karibu na Wana Wao?
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Novemba 1
    • 1. KUKOSA WAKATI: Katika nchi nyingi, akina baba ndio hufanya kazi ili kupata riziki kwa ajili ya familia. Mara nyingi kazi yao inawalazimu kuwa mbali na nyumbani saa nyingi kila siku. Katika maeneo mengine, akina baba wanatumia wakati mchache sana pamoja na watoto wao. Kwa mfano, utafiti fulani uliofanywa hivi karibuni huko Ufaransa ulionyesha kwamba akina baba katika nchi hiyo wanatumia chini ya dakika 12 kila siku kuwatunza watoto wao.

      FIKIRIA HILI: Unatumia muda gani pamoja na mwana wako? Kwa juma moja au majuma mawili yanayofuata, kwa nini usiandike jumla ya wakati unaotumia pamoja naye kila siku. Huenda matokeo yakakushangaza.

  • Akina Baba Wanawezaje Kuwa na Uhusiano wa Karibu na Wana Wao?
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Novemba 1
    • Na unawezaje kupata wakati wa kuwa pamoja naye?

      Kila inapowezekana, mhusishe mwana wako katika shughuli zako za kila siku. Kwa mfano, kama unafanya kazi fulani nyumbani, mwombe akusaidie. Mpe mvulana wako ufagio mdogo au jembe dogo. Bila shaka, mwana wako atafurahia kufanya kazi pamoja nawe kwa sababu anakuona kuwa shujaa na angependa kukuiga. Huenda ukachukua muda mrefu zaidi kumaliza kazi hiyo; lakini utaimarisha uhusiano kati yenu, na utamfundisha mwana wako mazoea mazuri ya kazi. Zamani, Biblia iliwatia moyo akina baba wawahusishe watoto wao katika shughuli zao za kila siku na kutumia pindi hizo kuzungumza nao na kuwafundisha. (Kumbukumbu la Torati 6:6-9) Bado mashauri hayo yanafaa.

      Zaidi ya kufanya kazi pamoja na mvulana wako, tafuta wakati wa kucheza pamoja naye. Kucheza kunatokeza nafasi za kujifurahisha na pia kufanya mambo mengine. Utafiti unaonyesha kwamba akina baba wanapocheza na watoto wao, jambo hilo huwatia moyo watoto wawe jasiri zaidi.

      Akina baba wanapocheza pamoja na watoto wao wanapata fursa nyingine muhimu zaidi. Mtafiti Michel Fize anasema hivi: “Mvulana anawasiliana vyema zaidi na baba yake wanapocheza pamoja.” Wanapocheza, baba anaweza kumwonyesha mwana wake kwamba anampenda kupitia maneno na matendo. Kwa kufanya hivyo, anamfundisha mwana wake jinsi ya kuwapenda wengine pia. “Wakati mwanangu alipokuwa bado mtoto,” anasema André, baba anayeishi huko Ujerumani, “tulicheza pamoja mara nyingi. Nilimkumbatia, na akajifunza kunionyesha upendo pia.”

      Wakati wa kulala ni kipindi kingine ambacho baba anaweza kuimarisha upendo kati yake na mwana wake. Msomee hadithi kwa ukawaida, na umsikilize anapoeleza kuhusu mambo aliyofurahia na yaliyomhangaisha siku hiyo. Ukifanya hivyo, itakuwa rahisi zaidi kwake kuendelea kuwasiliana nawe anapoendelea kukua.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki