-
Matatizo ya Pekee ya Familia za KamboMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Baba mmoja wa kambo aliungama: “Kwa kweli sikuwa tayari kushughulika na matatizo yote yanayohusiana na kulea watoto wangu wa kambo. Niliingia katika hali hiyo nikifikiri kwamba kwa kuwa sasa nilikuwa nimeoa mama yao, nilikuwa baba yao. Kwangu, hilo lilionekana kuwa jambo lisilo gumu sana! Sikuelewa upendo ambao watoto hao walikuwa nao kwa baba yao halisi, nami nilifanya makosa mengi sana.”
-
-
Familia za Kambo Zinaweza KufanikiwaMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Mwanamume mmoja aliyepata kuwa baba wa kambo afafanua matatizo yake hasa: “Mara nyingi nilihangaikia hisia zangu mno nisiweze kuchanganua hisia-moyo za watoto wangu wa kambo au hata za mke wangu. Ilinibidi nijifunze kutokuwa na hisia nyepesi mno. Jambo muhimu zaidi ni kwamba nilijifunza kuwa mnyenyekevu.” Upendo ulimsaidia kufanya marekebisho yaliyohitajika.
Mzazi Halisi
Upendo waweza kusaidia katika kushughulika na uhusiano wa watoto pamoja na baba yao halisi ambaye sasa hayupo. Baba wa kambo afunua siri hii: “Nilitaka watoto wangu wa kambo wanipende zaidi ya vile walivyompenda baba yao halisi. Walipomtembelea baba yao halisi, sikuweza kukinza kishawishi cha kumchambua. Waliporudi baada ya kuwa na wakati mzuri pamoja naye, nilihisi vibaya sana. Walipokuwa na wakati mbaya, nilifurahi. Kwa kweli nilihofia kupoteza shauku yao kwangu. Jambo lililokuwa gumu zaidi ni kung’amua na kukubali umuhimu wa fungu la baba halisi katika maisha ya watoto wangu wa kambo.”
Upendo wa kweli ulimsaidia baba huyo wa kambo kukabili uhakika wa kwamba halikuwa jambo la akili kutarajia kupendwa “mara moja.” Hakupaswa kuhisi amekataliwa wakati watoto walipokosa kumkubali mara moja. Alikuja kung’amua kwamba huenda asiweze kamwe kuchukua kabisa mahali pa baba halisi katika mioyo ya watoto wake. Hao watoto walimjua mwanamume huyo tangu walipokuwa wachanga kabisa, ilhali huyo baba wa kambo alikuwa mtu mpya ambaye ingembidi ajitahidi ili apate kupendwa na watoto hao. Mtafiti Elizabeth Einstein adhihirisha jambo linalowapata watu wengi anaposema hivi: “Mahali pa baba halisi hapawezi kamwe kuchukuliwa na mwingine—kamwe. Hata mzazi aliyekufa au aliyewaacha watoto huendelea kuwa na ushawishi muhimu katika maisha ya watoto hao.”
-
-
Familia za Kambo Zinaweza KufanikiwaMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Mzee mmoja Mkristo asimulia kwamba mara nyingi ilikuwa vigumu kuwaamsha watoto wake wa kambo Jumapili asubuhi ili washiriki katika ibada ya kutaniko. Badala ya kuwakemea vikali, alijaribu kuwa mwenye fadhili. Aliamka mapema, akatayarisha kiamsha-kinywa, kisha akapelekea kila mmoja wao kinywaji chenye joto. Tokeo likawa kwamba walielekea zaidi kusikiza ombi lake la kuwataka waamke.
-
-
Familia za Kambo Zinaweza KufanikiwaMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Namna gani ikiwa baba ndiye mzazi wa kambo? Je, Biblia haisemi kwamba baba ndiye kichwa cha familia? Ndiyo. (Waefeso 5:22, 23; 6:1, 2) Hata hivyo, huenda baba wa kambo akataka kumwachia mke daraka la kutoa nidhamu kwa muda mfupi, hasa ikiwa nidhamu hiyo yahusisha kutia adhabu. Huenda akawaruhusu watoto watii ‘sheria ya mama yao’ huku akiwawekea msingi wa ‘kusikiliza nidhamu ya baba yao [mpya].’ (Mithali 1:8; 6:20; 31:1) Ushuhuda waonyesha kwamba, mwishowe, jambo hilo halipingi kanuni ya ukichwa. Kwa kuongezea, baba mmoja wa kambo alisema: “Nilikumbuka kwamba nidhamu hutia ndani kuonya kwa upole, kusahihisha, na kukaripia. Kwa kawaida nidhamu huwa na matokeo inapotolewa katika njia ya haki, yenye upendo, na yenye huruma na kutegemezwa kwa kielelezo cha wazazi.”
-
-
Familia za Kambo Zinaweza KufanikiwaMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
Mama mmoja aliyeolewa tena asimulia: “Jambo lililo gumu zaidi kwa mama ni kuona baba wa kambo akiwatia watoto wake nidhamu, hasa ikiwa yeye ahisi kwamba anatenda kwa haraka-haraka au ni mwenye ubaguzi. Hilo humvunja moyo mama, naye hutaka kuwatetea watoto wake. Nyakati kama hizo, ni vigumu kuendelea kuwa mtiifu kwa mume wako na kumwunga mkono.
“Pindi moja, wavulana wangu wawili, wenye umri wa miaka 12 na 14, waliomba baba yao wa kambo ruhusa ya kufanya kitu fulani. Yeye alikataa mara moja, kisha akaondoka chumbani bila kuwapa wavulana hao fursa yoyote ya kueleza ni kwa nini ombi hilo lilikuwa muhimu kwao. Wavulana hao walikuwa tayari kulia, nami niliduwaa. Mvulana mwenye umri mkubwa zaidi alinitazama na kusema: ‘Mama, umeona vile amefanya?’ Nikajibu: ‘Ndiyo, nimeona. Lakini yeye bado ni kichwa cha nyumba hii, na Biblia hutuambia tustahi ukichwa.’ Walikuwa wavulana wazuri nao walikubaliana na jambo hilo na kutulia kidogo. Jioni hiyohiyo, nilimweleza mume wangu juu ya mambo hayo, naye aling’amua kwamba alikuwa ametumia mamlaka kupita kiasi. Alienda moja kwa moja chumbani mwa wavulana hao na kuwaomba radhi.
“Tulijifunza mengi kutokana na tukio hilo. Mume wangu alijifunza kusikiliza kabla ya kufanya maamuzi. Nilijifunza kuunga mkono kanuni ya ukichwa, hata linapokuwa jambo lenye kunitia uchungu. Wavulana walijifunza umuhimu wa kuwa watiifu. (Wakolosai 3:18, 19) Nao uombaji radhi wenye kuhisiwa moyoni wa mume wangu ukatufunza sote somo muhimu la unyenyekevu. (Mithali 29:23) Leo, wana hao wawili ni wazee Wakristo.”
-
-
Familia za Kambo Zinaweza KufanikiwaMnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
-
-
(Bila shaka, baba wa kambo wapaswa kuwa waangalifu kuweka mipaka ifaayo wanaposhughulika na binti zao wa kambo na kutowatia wasiwasi.
-