-
Ninaweza Kupangaje Matumizi ya Pesa Zangu?Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
-
-
Yafuatayo ni mapendekezo mengine ambayo yanaweza kukusaidia ikiwa una kadi ya mkopo.
● Andika orodha ya vitu unavyonunua na uilinganishe na taarifa ya akaunti ya kila mwezi ili uwe na hakika kwamba umetozwa tu vitu ulivyonunua.
● Lipa gharama unazodaiwa za kadi ya mkopo bila kuchelewa. Ikiwezekana, lipa kiasi chote.
● Uwe mwangalifu unapotoa nambari ya kadi yako ya mkopo na tarehe ya mwisho ya kadi hiyo kwenye simu au katika Intaneti.
● Epuka kutumia kadi ya mkopo kama njia rahisi ya kupata pesa taslimu. Kwa kawaida, kutoa pesa kwa njia hiyo hufanya utozwe kiwango cha juu cha riba.
● Usimpe kamwe mtu yeyote kadi yako ya mkopo, hata awe rafiki yako.
-
-
Ninaweza Kupangaje Matumizi ya Pesa Zangu?Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
-
-
JE, WAJUA . . .?
Ikiwa kadi yako ya mkopo ina deni la dola 2,000, na unatozwa riba ya asilimia 18.5, nawe unalipa tu kiwango cha chini cha lazima kilichowekwa na kampuni, itakuchukua miaka 11 kumaliza deni lako na utalipa dola 1,934 za ziada zikiwa riba.
-