Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unapaswa Kuwa Wapi Mwisho Unapokuja?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Mei 15
    • Walikuwa Mahali Panapofaa

      Tunasoma hivi kwenye 2 Petro 2:5-7 kuhusu kuokolewa kwa wazee wa ukoo, Noa na Loti: “[Mungu] hakujizuia kuuadhibu ulimwengu wa kale, bali alimlinda Noa, mhubiri wa uadilifu, akiwa salama pamoja na wengine saba alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiomwogopa Mungu; na kwa kuyageuza majiji ya Sodoma na Gomora kuwa majivu aliyahukumia adhabu, akiweka kielelezo kwa watu wasiomwogopa Mungu juu ya mambo yatakayokuja; naye alimkomboa Loti mwadilifu, aliyetaabishwa sana na kule kujitia mno katika mwenendo mpotovu kwa watu wanaokaidi sheria.”

      Noa aliokoka Gharika jinsi gani? Mungu alimwambia Noa hivi: “Mwisho wa wote wenye mwili umekuja mbele zangu, kwa maana dunia imejaa jeuri kwa sababu yao; na tazama mimi ninawaharibu pamoja na dunia. Jifanyie safina ya mti wenye utomvu.” (Mwa. 6:13, 14) Noa alijenga safina kama vile tu Yehova alivyomwagiza. Siku saba kabla ya Gharika kuanza, Yehova alimwagiza aingize wanyama ndani ya safina hiyo, kisha Noa angeingia ndani pamoja na washiriki wote wa familia yake. Siku ya saba, mlango ulifungwa, “na hiyo mvua kubwa juu ya dunia ikaendelea kwa siku 40, mchana na usiku.” (Mwa. 7:1-4, 11, 12, 16) Noa na familia yake “walichukuliwa salama kupitia maji.” (1 Pet. 3:20) Kuokolewa kwao kulitegemea wao kuwa ndani ya safina. Hakuna mahali pengine duniani ambapo pangekuwa salama.—Mwa. 7:19, 20.

  • Unapaswa Kuwa Wapi Mwisho Unapokuja?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Mei 15
    • Ni kweli kwamba, kuokoka kwa Noa kulitegemea kuwa ndani ya safina. Lakini kwa nini aliingia ndani ya safina? Ni kwa sababu alikuwa na imani na alikuwa mtiifu. Biblia inasema hivi: “Noa akafanya kulingana na yote ambayo Mungu alikuwa amemwamuru. Alifanya vivyo hivyo.” (Mwa. 6:22; Ebr. 11:7) Namna gani sisi? Je, tunafanya yote ambayo Mungu ametuamuru? Noa alikuwa pia “mhubiri wa uadilifu.” (2 Pet. 2:5) Kama Noa, je, sisi ni wenye bidii katika kazi ya kuhubiri, hata ikiwa watu wa eneo letu hawataki kutusikiliza?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki