-
Paradiso Katika Kisiwa cha MchangaAmkeni!—2006 | Machi
-
-
Maziwa na Misitu Isiyo ya Kawaida
Kwa kushangaza, katika kisiwa hicho, kuna maziwa 40 yenye maji safi juu ya marundo hayo ya mchanga. Baadhi ya maziwa hayo huonekana kana kwamba yamening’inia juu ya marundo marefu ya mchanga. Ni nini huzuia maji yasifyonzwe ndani ya mchanga? Majani, maganda, na matawi yaliyooza na kujikusanya chini ya maji.
Kisiwa hicho pia kina maziwa ambayo hujitokeza kwenye mashimo ya machanga yaliyo chini ya tabaka la maji. Maji safi huingia katika mashimo hayo na kufanyiza vidimbwi vyenye maji safi kabisa.
Kila mwaka, maziwa hayo hupata sentimeta 150 za mvua. Maji ambayo hayajaingia katika maziwa au kufyonzwa na mchanga hufanyiza vijito ambavyo huelekea baharini. Inakadiriwa kwamba kijito kimoja tu humwaga lita milioni tano za maji ndani ya Bahari ya Pasifiki kwa saa moja.
Kisiwa cha Fraser kina mimea mingi kwa sababu ya kuwa na maji mengi. Kwa kawaida, misitu ya mvua haiwezi kukua katika mchanga usiokuwa na rutuba. Lakini Kisiwa cha Fraser ni mojawapo ya sehemu chache ulimwenguni ambapo misitu ya mvua imenawiri kwenye mchanga. Kwa kweli, wakati mmoja msitu huo ulikuwa na miti mingi sana hivi kwamba miti yake ilitumiwa kutokeza mbao kwa zaidi ya miaka 100. Miti fulani yenye mbao ngumu ilipendwa sana. Mtaalamu mmoja wa misitu alisema hivi katika mwaka wa 1929: “Mtu anayetembea kwenye msitu huo huona ukuta wa miti mikubwa ya mbao yenye urefu wa meta 45 . . . Miti hiyo mikubwa ina kipenyo cha meta mbili hadi tatu.” Miti fulani ilitumiwa kutengeneza Mfereji wa Suez. Hata hivyo, leo watu hawaruhusiwi kukata miti katika Kisiwa cha Fraser.
-
-
Paradiso Katika Kisiwa cha MchangaAmkeni!—2006 | Machi
-
-
Jambo lisilo la kawaida—misitu ya mvua inayokua juu ya mchanga
-