-
Je, Misitu Yetu ya Mvua Itaokoka?Amkeni!—1998 | Mei 8
-
-
Mwanasayansi mmoja katika Taasisi ya Smithsonian katika Washington, D.C., alipendekeza kwamba asilimia 10 ya misitu ya mvua iliyoko iwekwe kando kwa ajili ya wazao, ili kulinda spishi nyingi iwezekanavyo. Kwa sasa ni karibu asilimia 8 zinazolindwa, lakini nyingi za hifadhi hizi au mbuga za kitaifa ni mbuga kwa jina tu, kwani hakuna fedha wala wafanyakazi wa kuzitunza. Kwa wazi, jambo fulani zaidi lapasa kufanywa.
Peter Raven, msemaji kwa ajili ya uhifadhi wa misitu ya mvua, aeleza: “Jitihada za kuokoa msitu wa mvua hutaka kuwe na uzalendo mpya baina ya mataifa, utambuzi wa kwamba watu kila mahali wanashiriki daraka katika masaibu ya dunia. Njia za kupunguza umaskini na njaa ulimwenguni pote lazima zipatikane. Mikataba mipya kati ya mataifa itahitaji kufanyizwa.”
Mapendekezo yake ni yenye kiasi kwa wengi. Kuokoa misitu ya mvua kwahitaji kitatuzi cha tufeni pote—kama vile tu hali nyingine zinazowakabili wanadamu. Tatizo linakuwa katika “kupata mikataba kati ya mataifa” kabla msiba mkubwa wa ulimwenguni pote haujatokea na kabla madhara hayajawa yasiyoweza kurekebishwa. Kama vile Peter Raven anavyodokeza, uharibifu wa msitu wa mvua wahusiana kwa ukaribu na matatizo mengine yasiyoweza kudhibitiwa kwa urahisi, ya nchi zinazoendelea, kama vile njaa na umaskini.
Kufikia sasa, jitihada za kimataifa zilizofanywa kuelekea matatizo haya hazikufanikiwa sana. Watu fulani huuliza, Je, siku moja mataifa yataweza kushinda tofauti zao ndogo za kitaifa kwa ajili ya manufaa ya wote, au kutafuta “uzalendo mpya baina ya mataifa” ni ndoto tu?
Historia haielekei kutoa misingi kwa ajili ya matumaini mema. Hata hivyo, jambo moja hupuuzwa mara nyingi—maoni ya Muumba wa msitu wa mvua. “Inapasa kuwekwa akilini kuwa tunaharibu sehemu ya Uumbaji,” Profesa wa Harvard Edward O. Wilson, atoa hoja, “kwa njia hiyo tukinyima vizazi vijavyo kile ambacho sisi wenyewe tuliachiwa kama urithi.”
Je, Muumba wa dunia atawaruhusu wanadamu kuiharibu kazi yake kabisa? Hilo lingekuwa lisiloeleweka.a Badala ya hivyo, Biblia hutabiri kwamba Mungu ‘atawaleta kwenye uangamizi wale wanaoiangamiza dunia.’ (Ufunuo 11:18) Mungu atatekelezaje kitatuzi chake? Anaahidi kusimamisha Ufalme—ufalme wa kimbingu wa mataifa yote—ambao utatatua matatizo yote ya dunia na ambao “hautaangamizwa milele.”—Danieli 2:44.
-
-
Je, Misitu Yetu ya Mvua Itaokoka?Amkeni!—1998 | Mei 8
-
-
a Kwa kupendeza, wanaotetea kuhifadhiwa kwa mali ya asili ambao lengo lao ni kuokoa spishi nyingi iwezekanavyo zilizo hatarini hueleza maadili yao kuwa “kanuni ya Noa,” kwani Noa aliagizwa kuweka katika safina “kila kilicho hai chenye mwili.” (Mwanzo 6:19) “Kuendelea kuwapo [kwa spishi] katika asili kwafikiriwa kuwa na haki isiyo na lawama ya kuendelea kuwako,” abisha mwanabiolojia David Ehrenfeld.
-