-
Kuenea kwa Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi za KidiniMnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
a Mshiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi ni mtu ashikamanaye sana na kanuni za msingi za kidini zenye kuhifadhi mambo na desturi za kale. Maana ya “harakati ya kufuata kanuni za msingi” itazungumziwa zaidi kikamili zaidi katika makala ifuatayo.
-
-
Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi za Kidini—Hiyo ni Nini?Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
HARAKATI ya kufuata kanuni za msingi ilianza wapi? Mwishoni mwa karne iliyopita, wanatheolojia wasioshikamana na desturi za zamani walikuwa wakibadili itikadi zao ili zilingane na uhakiki wa Biblia na nadharia za kisayansi, kama vile mageuzi. Tokeo ni kwamba, uhakika wa watu katika Biblia ulidhoofishwa. Viongozi wa kidini wenye kushikamana na desturi za zamani katika Marekani waliitikia kwa kuanzisha zile walizoita kanuni za msingi za imani.a Mapema katika karne ya 20, walichapisha mazungumzo juu ya kanuni hizo za msingi katika mfululizo wa mabuku wenye kichwa The Fundamentals: A Testimony to the Truth (Kanuni za Msingi: Ushuhuda wa Kweli). Usemi “harakati ya kufuata kanuni za msingi” watokana na kichwa hicho.
-
-
Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi za Kidini—Hiyo ni Nini?Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
a Zile ziitwazo kwa kawaida Hoja Tano za Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi, zilizofasiliwa mwaka wa 1895, zilikuwa “(1) upulizio wa kamili na ukamilifu wa Andiko; (2) uungu wa Yesu Kristo; (3) kuzaliwa kwa Kristo na bikira; (4) ufuniko wa badala wa Kristo juu ya msalaba; (5) ufufuo wa kimwili wa Kristo na kuja kwake kwa pili duniani, kibinafsi na kimwili.”—Studi di teologia (Masomo ya Kitheolojia).
-
-
Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi za Kidini—Hiyo ni Nini?Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
Leo, maneno “harakati ya kufuata kanuni za msingi za kidini” hutumiwa si kuhusu harakati za Kiprotestanti tu, bali pia kuhusu wale katika dini nyingine, kama vile Ukatoliki, Uislamu, Dini ya Kiyahudi, na Dini ya Hindu.
-
-
Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi za Kidini—Hiyo ni Nini?Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
Kumtambulisha Mshiriki wa Harakati ya Kufuata Kanuni za Msingi
Kwa kawaida harakati ya kufuata kanuni za msingi kidini ni jaribio la kuhifadhi zile zionwazo kuwa desturi au itikadi za kidini za awali za utamaduni fulani na kupinga ile ionwayo kuwa roho ya kilimwengu ya ulimwengu. Hilo si kusema kwamba washiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi hupinga mambo yote yaliyo ya kisasa. Baadhi yao hutumia njia za uwasiliano za kisasa kwa matokeo sana ili kuendeleza maoni yao. Lakini wanapiga vita dhidi ya kufanywa kilimwengu kwa jamii.b
Baadhi ya washiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi wanaazimia si kujihifadhia wenyewe tu muundo wa kidesturi wa mafundisho au wa njia ya maisha bali pia kulazimisha wengine waufuate, wapate kubadili miundo ya kijamii ili ipatane na itikadi za washiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi. Kwa hiyo, Mkatoliki aliye mshiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi, hatakazia tu upingaji wa utoaji-mimba. Yamkini atawasonga wanasheria wa nchi yake waendeleze sheria zinazokataza utoaji-mimba. Katika Poland, kulingana na gazeti la habari La Repubblica, ili sheria inayopinga utoaji-mimba ikubaliwe, Kanisa Katoliki liliongoza “‘vita’ ambayo katika hiyo lilitumia mamlaka na nguvu zalo zote.” Katika kufanya hivyo, wenye mamlaka wa kanisa walikuwa wakitenda sawa sana na washiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi. Ule Muungano wa Kikristo wa Kiprotestanti katika Marekani hupiga “vita” vya aina hiyohiyo.
Washiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi hutambulika hasa kwa masadikisho yao ya kidini yenye msingi imara. Hivyo, Mprotestanti aliye mshiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi atakuwa muungaji-mkono mwenye kusadikishwa wa ufafanuzi wa halisi wa Biblia, yamkini kutia ndani itikadi ya kwamba dunia iliumbwa katika siku sita halisi. Mkatoliki aliye mshiriki wa harakati ya kufuata kanuni za msingi hana shaka zozote juu ya ukamilifu wa papa.
-