-
Je, Kuna Matumaini Yoyote kwa Dunia?Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 1
-
-
Sayari Hatarini
Mnamo 2002 Taasisi ya Mazingira ya Stockholm inayoheshimiwa ilionya kwamba wanadamu wasipozuiwa kuiharibu dunia kwa sababu ya shughuli zao za kibiashara, hilo lingeanzisha “matukio ambayo yanaweza kugeuza sana hali ya hewa ya sayari yetu na mifumo ya ikolojia.” Ripoti hiyo iliendelea kusema kwamba umaskini ulimwenguni, ukosefu wa usawa, na kutumiwa sana kwa maliasili kunaweza kufanya wanadamu wakabiliane na “matatizo mbalimbali ya kimazingira, kijamii, na usalama.”
Katika 2005, shirika la Umoja wa Mataifa lilitoa ripoti ya uchunguzi wa miaka minne ya mazingira ya Dunia iliyoitwa Ukaguzi wa Milenia wa Mifumo ya Ikolojia. Uchunguzi huo wa kina ulihusisha wataalamu zaidi ya 1,360 kutoka nchi 95. Ulitoa onyo hili kali: “Shughuli za wanadamu zinalemea sana utendaji wa asili wa Dunia hivi kwamba hatuwezi kutarajia mifumo ya ikolojia iendelee kutegemeza uhai wa vizazi vijavyo.” Ripoti hiyo inaendelea kusema kwamba ili kuepuka msiba kunahitajiwa “mabadiliko makubwa katika sera, taasisi, na mazoea. Mabadiliko hayo hayapo kwa sasa.”
Anna Tibaijuka msimamizi mkuu wa Mradi wa Umoja wa Mataifa Unaoshughulikia Makao, anasema kile ambacho watafiti wengi wanaamini. Anasema hivi: “Tukiendelea kufanya mambo kama kawaida, tutakuwa na wakati ujao mbaya.”
-
-
Hizi Ni Nyakati za HatariMnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 1
-
-
Ripoti za karibuni zinasema: “Shughuli za wanadamu zimetokeza uwezekano wa kutoweka kwa jamii nyingi za mimea na wanyama.” “Asilimia 60 hivi ya utendaji wa asili wa mifumo ya ikolojia ya dunia unaotegemeza uhai unapungua.”—Ukaguzi wa Milenia wa Mifumo ya Ikolojia.
“Gesi zinazoongeza joto ulimwenguni zinazotokezwa na wanadamu zinahatarisha hali ya hewa ya Dunia, na hivyo kufanya kuwe na uwezekano wa kuathiriwa vibaya kwa sayari hii.”—NASA, Taasisi ya Goddard ya Uchunguzi wa Angani.
-