Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Twatambuliwa kwa Mwenendo Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kama vile imeonyeshwa katika vichapo vyao, hamna amri hususa katika Biblia isemayo, Ni lazima usicheze kamari. Lakini tunda la kucheza kamari ni baya daima, na tunda hilo bovu limefichuliwa na Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwa nusu karne. Zaidi ya hilo, magazeti hayo yameonyesha kwamba kucheza kamari kwa namna yoyote kwahusu mitazamo ambayo Biblia huonya dhidi yayo. Kwa kielelezo, kupenda fedha: “Kupenda fedha ni mzizi wa mambo mabaya ya namna zote.” (1 Tim. 6:10, NW) Na ubinafsi: “Wala usitamani . . . kitu cho chote alicho nacho jirani yako.” (Kum. 5:21; linganisha 1 Wakorintho 10:24.) Pia pupa: “Mkome kuchangamana katika ushirika pamoja na yeyote aitwaye ndugu ambaye ni . . . mwenye pupa.” (1 Kor. 5:11, NW) Kwa kuongezea, Biblia huonya juu ya kuomba “Bahati [Njema]” kana kwamba ni kani fulani yenye nguvu zipitazo zile za asili ambayo ingeweza kutoa mapendeleo. (Isa. 65:11)

  • Twatambuliwa kwa Mwenendo Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kucheza kamari hakujapata wakati wowote kuwa suala kubwa miongoni mwa Mashahidi wa Yehova. Wanajua kwamba badala ya kusitawisha roho ya pato kwa hasara ya wengine, Biblia huwatia moyo kufanya kazi kwa mikono yao, kuwa waaminifu katika kutunza waliyokabidhiwa, kuwa wakarimu, kushiriki vitu na wale wenye uhitaji. (Efe. 4:28; Luka 16:10; Rum. 12:13; 1 Tim. 6:18)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki