-
Je, Biblia Inashutumu Kucheza Kamari?Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
-
-
Mbali na kushinda au kupoteza katika mchezo wa kamari, kuna “mtego” mwingine unaopaswa kuepukwa. “Wale ambao wameazimia kuwa matajiri huanguka katika jaribu na mtego na tamaa nyingi za kijinga na zenye kudhuru, ambazo hutumbukiza watu katika maangamizi na uharibifu,” linasema Neno la Mungu. (1 Timotheo 6:9) Mtego unakusudiwa kumnasa mnyama. Watu wengi waliokusudia kutumia pesa kidogo tu katika mchezo wa kamari au kucheza mara chache tu, wamenaswa kabisa na zoea hilo wasiweze kujinasua. Mchezo wa kamari umefanya watu wapoteze kazi, waumize wapendwa wao, na umevunja familia.
-
-
Je, Biblia Inashutumu Kucheza Kamari?Mnara wa Mlinzi—2011 | Machi 1
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 13]
Msisimko wa Kushinda
Je, kucheza kamari ni zoea linaloweza kumnasa mtu, na kwa urahisi kumfanya awe mchezaji sugu? Baada ya kufanya uchunguzi kuhusu jinsi wachezaji wa kamari wanavyohisi baada ya kushinda au kupoteza, Dakt. Hans Breiter anasema kwamba “msisimko ambao mtu hupata katika ubongo baada ya kushinda pesa katika mchezo wa kamari, unakuwa sawa na ule ambao mtumiaji wa kokeini hupata baada ya kuitumia.”
-