Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Lile “Hekalu” na Yule “Mkuu” Leo
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
    • 3. Twajifunza nini kutokana na dari refu na michoro iliyo ukutani katika vijia vya kuingia hekaluni?

      3 Wazia kwamba tunazuru hekalu hilo la kimaono. Twakaribia na kupanda vipandio saba hadi kwenye moja la hayo malango makubwa mno. Tukiwa ndani ya kijia hicho cha kuingilia, twatazama juu kwa kuduwaa. Dari lake lina urefu wa meta 30 kwenda juu! Hivyo, twakumbushwa kwamba viwango vya kuingia katika mpango wa Yehova wa ibada ni vya juu sana. Miali ya nuru inayopenyeza kutoka madirishani yamulika michoro ya mitende iliyo ukutani, ambayo hutumiwa katika Maandiko kufananisha unyofu. (Zaburi 92:12; Ezekieli 40:14, 16, 22) Mahali hapo patakatifu ni pa wale walio wanyofu kiadili na kiroho. Kwa kupatana na hilo, twataka kubaki tukiwa wanyofu ili ibada yetu ikubalike kwa Yehova.—Zaburi 11:7.

      4. Ni nani wanaozuiwa kuingia hekaluni, na hilo latufunza nini?

      4 Kando-kando ya pande zote za kijia hicho, pana vyumba vitatu vya walinzi. Je, hao walinzi wataturuhusu tuingie ndani ya hekalu? Yehova amwambia Ezekieli kwamba hapana mgeni ambaye “moyo wake haukutahiriwa” awezaye kuingia. (Ezekieli 40:10; 44:9) Hilo lamaanisha nini? Lamaanisha kwamba Mungu hukubali tu wale wanaopenda sheria zake na kuishi kulingana nazo wamwabudu. (Yeremia 4:4; Waroma 2:29) Yeye huwakaribisha watu wa aina hiyo katika hema lake la kiroho, nyumba yake ya ibada. (Zaburi 15:1-5) Tangu ibada safi irudishwe mwaka wa 1919, tengenezo la kidunia la Yehova limetegemeza na kufafanua sheria zake za adili hatua kwa hatua. Wale wanaokataa kutii kimakusudi hawakubaliwi tena kushirikiana na watu wake. Leo, lile zoea linalotegemea Biblia la kutenga na ushirika wakosaji wasiotubu limesaidia kudumisha ibada yetu ikiwa safi na yenye utakato.—1 Wakorintho 5:13.

  • Lile “Hekalu” na Yule “Mkuu” Leo
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
    • 8. Ni nani waingiao malango yanayoelekea kwenye ua wa ndani, na malango hayo yatukumbusha nini?

      8 Tunapotembea kuvuka ua wa nje, huenda tukaona kwamba kuna malango matatu ya kuingia kwenye ua wa ndani; malango ya ndani yako kwenye mpangilio mmoja na malango ya nje, nayo ni yenye kipimo kimoja na hayo ya nje. (Ezekieli 40:6, 20, 23, 24, 27) Ni makuhani tu wanaoweza kuingia katika ua wa ndani. Malango ya ndani yatukumbusha kwamba ni lazima watiwa-mafuta wafikie viwango na sheria za kimungu, viwango na sheria hizohizo huwaongoza Wakristo wote wa kweli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki