Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Kutoka Katika Kitabu cha Mwanzo—I
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Januari 1
    • WANADAMU WAINGIA KATIKA KIPINDI KIPYA

      (Mwanzo 8:1–11:9)

      Wanadamu wanaingia katika kipindi kipya baada ya ulimwengu uliotangulia Gharika kutoweka. Wanadamu wanaruhusiwa kula nyama, lakini wanaamuriwa wajiepushe na damu. Yehova anaruhusu adhabu ya kifo kwa wauaji naye anaanzisha agano la upinde wa mvua, akiahidi kwamba hataleta kamwe Gharika nyingine. Wana watatu wa Noa wanakuwa mababu wa jamii yote ya kibinadamu, lakini kitukuu wake Nimrodi anakuwa “mwindaji mwenye nguvu kwa kumpinga Yehova.” Badala ya kusambaa na kuijaza dunia, watu wanaamua kujenga mnara na jiji linaloitwa Babeli ili kujifanyia jina maarufu. Makusudi yao yanazuiwa pale Yehova anapoivuruga lugha yao na kuwatawanya duniani kote.

  • Mambo Makuu Kutoka Katika Kitabu cha Mwanzo—I
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Januari 1
    • Neno la Mungu Linaweza Kuwa na Nguvu

      Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo ndiyo tu ina masimulizi sahihi kuhusu historia ya mapema ya mwanadamu. Sehemu hiyo inatusaidia kufahamu kusudi la Mungu la kuwaweka wanadamu duniani. Inatia moyo kama nini kuona kwamba hakuna jitihada za binadamu, kama zile za Nimrodi, zinazoweza kuzuia kusudi hilo lisitimizwe!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki