Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Kutoka Kitabu cha Mwanzo—II
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Januari 15
    • ABRAHAMU AWA RAFIKI YA MUNGU

      (Mwanzo 11:10–23:20)

      Miaka 350 hivi baada ya Gharika, mtu anayekuja kuwa wa pekee sana kwa Mungu anazaliwa katika ukoo wa Shemu, mwana wa Noa. Jina lake ni Abramu, ambalo baadaye linabadilishwa kuwa Abrahamu. Kwa amri ya Mungu, Abramu anaondoka jiji la Uru la Wakaldayo na kuwa mkaaji wa mahema katika nchi ambayo Yehova anamwahidi angempa yeye na wazao wake. Kwa sababu ya imani na utii wake, Abrahamu anakuja kuitwa “rafiki ya Yehova.”—Yakobo 2:23.

      Yehova anachukua hatua dhidi ya wakaaji wa Sodoma na majiji yaliyo karibu, huku akimhifadhi Loti na binti zake. Ahadi ya Mungu inatimizwa wakati Isaka mwana wa Abrahamu anapozaliwa. Miaka kadhaa baadaye, imani ya Abrahamu inajaribiwa wakati Yehova anapomwagiza amtoe mwana wake kuwa dhabihu. Abrahamu yu tayari kutii lakini malaika anamzuia. Bila shaka, Abrahamu ni mtu mwenye imani, naye anahakikishiwa kwamba kupitia uzao wake mataifa yote yatajibariki. Abrahamu anahuzunishwa sana na kifo cha Sara mke wake mpendwa.

  • Mambo Makuu Kutoka Kitabu cha Mwanzo—II
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Januari 15
    • YAKOBO ANA WANA 12

      (Mwanzo 24:1–36:43)

      Abrahamu anapanga ndoa ya Isaka na Rebeka, mwanamke ambaye anamwamini Yehova. Anazaa mapacha, Esau na Yakobo. Esau anadharau haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza na kuiuza kwa Yakobo, ambaye baadaye anapokea baraka ya baba yake. Yakobo anakimbilia Padan-aramu, ambako anaoa Lea na Raheli na kuchunga makundi ya wanyama wa baba yao kwa miaka 20 kabla ya kuondoka pamoja na familia yake. Kupitia Lea, Raheli, na wajakazi wake wawili, Yakobo ana wana 12 na binti mmoja. Yakobo anapigana mweleka na malaika naye anabarikiwa, na jina lake linabadilishwa kuwa Israeli.

  • Mambo Makuu Kutoka Kitabu cha Mwanzo—II
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Januari 15
    • YEHOVA AMBARIKI YOSEFU HUKO MISRI

      (Mwanzo 37:1–50:26)

      Wivu unafanya wana wa Yakobo wamuuze ndugu yao Yosefu kuwa mtumwa. Akiwa Misri, Yosefu anatiwa gerezani kwa sababu anadumisha viwango vya Mungu vya maadili kwa ujasiri na kwa uaminifu. Baada ya muda, anatolewa gerezani ili kumfasiria Farao ndoto zake, ambazo zinatabiri miaka saba ya shibe na miaka saba ya njaa. Baadaye, Yosefu anawekwa kuwa msimamizi wa chakula wa Misri. Ndugu zake wanakuja Misri kutafuta chakula kwa sababu ya njaa. Familia hiyo inaungana tena na kuishi katika nchi yenye rutuba ya Gosheni. Kabla tu ya kufa, Yakobo anawabariki wana wake na kutamka unabii unaotoa tumaini hakika la baraka nyingi za wakati ujao. Mwili wa Yakobo unapelekwa Kanaani ukazikwe. Yosefu anapokufa akiwa na umri wa miaka 110, mwili wake unatiwa dawa, ili mwishowe usafirishwe hadi Nchi ya Ahadi.—Kutoka 13:19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki