Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kweli Watu wa Nyakati za Biblia Waliishi Kwa Muda Mrefu Sana?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Desemba 1
    • Watu Walioishi Muda Mrefu

      Kitabu cha Mwanzo kinazungumza kuhusu wanaume saba walioishi zaidi ya miaka 900, wote wakiwa wamezaliwa kabla ya Gharika ya siku za Noa. Watu hao ni Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Yaredi, Methusela, na Noa. (Mwanzo 5:5-27; 9:29) Huenda watu wengi wasiwafahamu wengi wa wanaume hao, lakini wote walikuwa miongoni mwa vizazi kumi vya kwanza katika historia ya mwanadamu. Methusela anajulikana kwa kuishi miaka mingi zaidi, yaani, miaka 969!

      Biblia inataja watu wengine 25 ambao waliishi miaka mingi zaidi ya ile ambayo watu wanaishi leo. Baadhi yao waliishi miaka 300, 400, hata miaka 700 au zaidi. (Mwanzo 5:28-31;

  • Je, Kweli Watu wa Nyakati za Biblia Waliishi Kwa Muda Mrefu Sana?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Desemba 1
    • Je, Wakati Ulipimwa kwa Njia Tofauti?

      Wengine wamedai kwamba wakati ulipimwa kwa njia tofauti nyakati hizo na kwamba ule uliokuwa ukiitwa mwaka kwa kweli ulikuwa mwezi mmoja. Hata hivyo, uchunguzi wa masimulizi ya kitabu cha Mwanzo, unaonyesha waziwazi kwamba watu wa nyakati zile walipima wakati kama tu tunavyofanya leo. Fikiria mifano miwili. Katika simulizi la Gharika, tunasoma kwamba Gharika hiyo ilianza wakati Noa alipokuwa na miaka 600, katika “mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi.” Kisha linaendelea kusema kwamba maji yaliifunika dunia kwa siku 150 na kwamba “katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina i[li]tua kwenye milima ya Ararati.” (Mwanzo 7:11, 24; 8:4) Kwa hiyo, kipindi hicho cha miezi mitano—kuanzia siku ya 17 ya mwezi wa pili mpaka siku ya 17 ya mwezi wa saba mwaka huo—ni siku 150. Bila shaka, dai la kwamba mwaka mmoja ulikuwa ni mwezi mmoja kwa kweli halina msingi.

      Fikiria mfano wa pili. Kulingana na Mwanzo 5:15-18, Mahalaleli alimzaa mwana wake akiwa na umri wa miaka 65, na akaendelea kuishi kwa miaka 830, na kufa akiwa na umri wa miaka 895. Pia Enoko mjukuu wake alimzaa mwana akiwa na umri wa miaka 65. (Mwanzo 5:21) Ikiwa kwa kweli mwaka ulikuwa sawa na mwezi mmoja, basi wanaume hao wawili walizaa wakiwa na miaka mitano tu. Je, hilo linalopatana na akili?

  • Je, Kweli Watu wa Nyakati za Biblia Waliishi Kwa Muda Mrefu Sana?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Desemba 1
    • Miaka mingi ambayo watu wa kabla ya Gharika waliishi inathibitisha kwamba mwili wa mwanadamu una uwezo wa ajabu wa kuishi muda marefu sana. Teknolojia ya kisasa imewawezesha wanasayansi kuchunguza vizuri mwili wa mwanadamu na jinsi ulivyobuniwa kwa njia ya ajabu, kutia ndani uwezo wake wa ajabu wa kujifanyiza upya na kujiponya wenyewe. Wamefikia uamuzi gani? Mwili wa mwanadamu unaweza kuishi milele. Profesa wa Kitiba Tom Kirkwood, anasema, “[Kuzeeka] ni moja kati ya mambo magumu yasiyoweza kufafanuliwa katika sayansi ya kitiba.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki