-
Kwa Nini Hali ya Hewa Imebadilika?Amkeni!—2003 | Agosti 8
-
-
Mambo Yanayoweza Kusababishwa na Ongezeko la Joto
Ongezeko la gesi hizo ambalo limetokana na shughuli za wanadamu limesababisha nini? Wanasayansi wengi sasa wanakubali kwamba joto la dunia limeongezeka. Limeongezeka kiasi gani? Ripoti ya kamati ya IPCC ya mwaka wa 2001 inasema hivi: “Joto la uso wa dunia limeongezeka kwa nyuzi 0.4 Selsiasi hadi 0.8 Selsiasi tangu mwishoni mwa karne ya 19.” Watafiti wengi wanaonelea kwamba huenda ongezeko hilo dogo ndilo linalosababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.
Ama kwa hakika, mfumo wa hali ya hewa duniani ni tata sana, na wanasayansi hawawezi kueleza kwa uhakika athari za ongezeko la joto duniani. Hata hivyo, wengi wanaamini kwamba kumekuwa na ongezeko la mvua upande wa kaskazini wa dunia, ukame huko Asia na Afrika, na kwamba El Niño imetukia mara nyingi zaidi katika Pasifiki.
-
-
Kwa Nini Hali ya Hewa Imebadilika?Amkeni!—2003 | Agosti 8
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 6]
“Je, Ongezeko la Joto Duniani Linadhuru Afya?”
Swali hilo lenye kuvuta fikira lilizushwa katika makala moja ya gazeti Scientific American. Makala hiyo ilitabiri kwamba ongezeko la joto duniani “litafanya magonjwa mengi hatari yaenee na kutokea mara nyingi zaidi.” Kwa mfano, katika maeneo fulani, “inakadiriwa kwamba idadi ya vifo vinavyosababishwa na joto kali itaongezeka maradufu kufikia mwaka wa 2020.”
Haijulikani waziwazi kama ongezeko la joto duniani linaweza kuleta magonjwa ya kuambukiza. “Inasemekana kwamba magonjwa yanayoletwa na mbu yataongezeka,” kwani mbu “huzaana kwa wingi na huuma zaidi joto linapoongezeka. . . . Hivyo, joto linapoongezeka katika maeneo mbalimbali, huenda mbu wakaingia hata mahali ambapo hawakuwepo zamani, na kueneza magonjwa.”
Mwishowe, mafuriko na ukame zinaweza kuchafua maji. Ama kweli, ongezeko la joto duniani ni jambo linalopaswa kutiliwa maanani.
-