-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na bado malaika mwingine [wa sita] akaibuka kutoka katika madhabahu na yeye alikuwa na mamlaka juu ya moto. Na yeye akaita kwa sauti kubwa kwa mmoja ambaye alikuwa na mundu mkali, akisema: ‘Tia ndani mundu wako mkali na kukusanya vichala vya mzabibu wa dunia, kwa sababu zabibu zao zimepata kuiva.’” (Ufunuo 14:17, 18, NW)
-
-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
26. Ni nini ulio “mzabibu wa dunia”?
26 Lakini ni nini ulio “mzabibu wa dunia”? Katika Maandiko ya Kiebrania, taifa la Kiyahudi lilisemwa kuwa mzabibu wa Yehova. (Isaya 5:7; Yeremia 2:21) Hali kadhalika, Yesu Kristo pamoja na wale ambao watatumikia pamoja na yeye katika Ufalme wa Mungu wanasemwa kuwa mzabibu. (Yohana 15:1-8) Katika mazingira haya, tabia ya maana ya mzabibu ni kwamba unazaa tunda, na mzabibu wa kweli wa Kikristo umezaa tunda jingi kwa sifa ya Yehova. (Mathayo 21:43) Kwa hiyo, lazima “mzabibu wa dunia,” uwe, si huu mzabibu halisi, bali mwigo wa Shetani wa huo mzabibu, mfumo wake mfisadi uonekanao wa kiserikali juu ya aina ya binadamu, pamoja na “vichala” mbalimbali vyao vya tunda la roho waovu ambalo limezaliwa kwa muda wa karne zilizopita. Babuloni Mkubwa, ambaye Jumuiya ya Wakristo yenye kuasi imani ndiyo yenye kutokeza zaidi, ametumia uvutano mkubwa juu ya huu mzabibu wenye sumu.—Linga Kumbukumbu 32:32-35.
27. (a) Kunatukia nini wakati malaika mwenye mundu anapokusanya “mzabibu wa dunia”? (b) Ni unabii gani katika Maandiko ya Kiebrania unaoonyesha kadiri ya vuno hilo?
27 Lazima hukumu itekelezwe! “Na malaika akatia mundu wake ndani ya dunia na kukusanya mzabibu wa dunia, na yeye akavurumisha huo ndani ya shinikizo la divai kubwa la kasirani ya Mungu. Na shinikizo la divai likakanyagwa nje ya jiji, na damu ikaja nje ya shinikizo la divai mpaka juu kabisa kwenye hatamu za wale farasi, kwa kitalifa cha farlong’i elfu moja mia sita.” (Ufunuo 14:19, 20, NW) Ghadhabu ya Yehova dhidi ya mzabibu huu imetangazwa kwa muda mrefu uliopita. (Sefania 3:8) Unabii katika kitabu cha Isaya hauachi shaka lolote kwamba mataifa mazima mazima yataharibiwa wakati shinikizo la divai linapokanyagwa. (Isaya 63:3-6) Yoeli vilevile alitoa unabii kwamba “umati wa watu” mkubwa, mataifa mazima mazima, yangekanyagwa na kuharibiwa katika “shinikizo la divai,” katika “uwanda-bonde wa uamuzi.” (Yoeli 3:12-14, NW) Kwa kweli, ni vuno kubwa sana ambalo mfano walo hautatukia tena kamwe! Kulingana na njozi ya Yohana, si zabibu tu zinazovunwa bali mzabibu wote mzima wa ufananisho unakatwa na kutupwa ndani ya shinikizo la divai ukanyagwe. Hivyo mzabibu wa dunia utang’olewa wote na hautaweza kamwe kukua tena.
28. Ni nani wanaokanyaga mzabibu wa dunia, na humaanisha nini kwamba shinikizo la divai ‘linakanyagwa nje ya jiji’?
28 Mkanyago wa kinjozi hufanywa na farasi, kwa kuwa damu inayokanyagwa kutoka mzabibu inafika kwenye “zile hatamu za wale farasi.” Kwa kuwa usemi “wale farasi” mara nyingi hurejezea utendaji wa kivita, lazima huu uwe wakati wa vita. Yale majeshi ya kimbingu ambayo hufuata Yesu kwenye vita ya mwisho dhidi ya mfumo wa mambo wa Shetani wanasemwa kuwa wanakanyaga “shinikizo la divai ya kasirani ya hasira-kisasi ya Mungu Mweza Yote.” (Ufunuo 19:11-16, NW) Kwa wazi hawa ndio wanaokanyaga “mzabibu wa dunia.” Hilo shinikizo la divai ‘hukanyagwa nje ya jiji,’ yaani, nje ya Sayuni la kimbingu. Kweli kweli, inafaa huo mzabibu wa dunia ukanyagwe duniani. Lakini pia ‘utakanyagwa nje ya jiji, hivi kwamba hakuna dhara litakalopata wale wabakio wa mbegu ya mwanamke, wanaowakilisha Sayuni la kimbingu duniani. Hawa pamoja na umati mkubwa watafichwa kwa usalama ndani ya mpango wa Yehova wa tengenezo la kidunia.—Isaya 26:20, 21.
29. Damu kutoka shinikizo la divai ina kina cha kadiri gani, hufika kwenye kitalifa gani, na hayo yote huonyesha nini?
29 Njozi hii iliyo wazi sana ina ulingano na kule kupondwa-pondwa kwa falme za dunia kwa njia ya jiwe la Ufalme kunakoelezwa kwenye Danieli 2:34, 44. Kutakuwako kuuliwa mbali kabisa. Ule mto wa damu kutoka shinikizo la divai ni wenye kina sana, mpaka kwenye hatamu za wale farasi, na hufikia kitalifa cha farlong’i 1,600.a Tarakimu hii kubwa, inayotokezwa kwa kuzidisha mraba wa nne kwa mraba wa kumi (4 x 4 x 10 x 10), kwa mkazo huwasilisha ujumbe wa kwamba ithibati ya uharibifu itahusisha ndani dunia yote. (Isaya 66:15, 16) Uharibifu utakuwa kamili na usiogeuzika. Hasha, la hasha, mzabibu wa dunia wa Shetani hautatia mzizi tena!—Zaburi 83:17, 18.
30. Ni matunda gani ya mzabibu wa Shetani, na azimio letu limepaswa kuwa nini?
30 Sisi tukiwa tunaishi ndani sana ya wakati wa mwisho, hiyo njozi ya haya mavuno mawili ni yenye maana sana. Tunaloweza kufanya tu ni kutazama pande zetu zote tuone yaliyo matunda ya mzabibu wa Shetani. Utoaji-mimba na namna nyinginezo za uuaji kimakusudi; ugoni-jinsia-moja, uzinzi, na namna nyingine za utovu wa adili, utovu wa haki, utovu wa shauku asilia—mambo yote kama hayo hufanya ulimwengu huu kuwa mbaya sana machoni pa Yehova. Mzabibu wa Shetani huzaa “tunda la pando lenye sumu na pakanga.” Mwendo wao wa uangamivu, wenye kuabudu sanamu hukosa kuheshimu Muumba mtukufu wa aina ya binadamu. (Kumbukumbu 29:18; 32:5; Isaya 42:5, 8, NW)
-