Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Pia alisafiri Ulaya katika 1891 ili kuona ni jambo gani lingeweza kufanywa ili kusogeza mbele kuenezwa kwa kweli huko. Safari hiyo ilimpeleka Ireland, Scotland, Uingereza, nyingi za nchi za bara la Ulaya, Urusi (lile eneo liitwalo sasa Moldova), na Mashariki ya Kati.

      Alifikia mkataa gani baada ya kuwasiliana na watu katika safari hiyo? “Sisi hatukuona kufunguka au utayari kwa ajili ya kweli katika Urusi . . . Hatukuona jambo lolote la kututia moyo tutumainie vuno lolote katika Italia au Uturuki au Austria au Ujerumani,” akaripoti. “Lakini Norway, Sweden, Denmark, Uswisi, na hasa Uingereza, Ireland, na Scotland, ni mashamba yaliyo tayari na yanangojea kuvunwa. Mashamba hayo yaonekana yakilia, Njooni huku mtusaidie!” Hiyo ilikuwa ile enzi ambayo Kanisa Katoliki lilikuwa lingali likikataza usomaji wa Biblia, wakati Waprotestanti wengi walikuwa wakiacha makanisa yao, na wengi, wakikatishwa tamaa na makanisa, walikuwa wakikataa Biblia kabisa.

      Ili kusaidia wale watu waliokuwa na njaa kiroho, baada ya safari ya Ndugu Russell katika 1891, jitihada zilizoongezwa zilifanywa kutafsiri fasihi katika lugha za Ulaya. Pia, mipango ilifanywa ili kuchapa na kuweka akiba ya fasihi katika London ili fasihi hizo ziweze kupatikana kwa urahisi kwa matumizi katika Uingereza. Shamba la Uingereza, lilithibitika kwelikweli kuwa tayari kuvunwa. Kufikia 1900, tayari kulikuwa makutaniko tisa na jumla ya Wanafunzi wa Biblia 138—miongoni mwao makolpota fulani wenye bidii. Wakati Ndugu Russell alipotembelea Uingereza tena katika 1903, watu elfu moja walikusanyika katika Glasgow ili kumsikia akihutubu juu ya “Matumaini na Matarajio ya Mileani,” 800 walihudhuria katika London, na wasikilizaji 500 kufikia 600 katika miji mingine.

  • Sehemu ya 1—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Ramani katika ukurasa wa 407]

      (See publication)

      Safari za Russell za kwenda kuhubiri Ulaya, kwa kawaida kupitia Uingereza

      1891

      1903

      1908

      1909

      1910 (mara mbili)

      1911 (mara mbili)

      1912 (mara mbili)

      1913

      1914

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki