Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Nywele Zako Zinakuhangaisha?
    Amkeni!—2002 | Agosti 8
    • Nywele hukua zaidi ya sentimeta moja kila mwezi, na ni mojawapo ya sehemu za mwili zinazokua haraka sana. Kama ukuzi wa nywele zote ungejumlishwa katika unywele mmoja, huo ungekua zaidi ya meta 20 kwa siku!

  • Je, Nywele Zako Zinakuhangaisha?
    Amkeni!—2002 | Agosti 8
    • [Sanduku/Mchoro katika ukurasa wa 27]

      UKUZI WA NYWELE

      Nywele hukua hatua kwa hatua. Hatua hizo ni hatua ya kukua, hatua fupi ya kubadilika kwa unywele, na ya kutokua. Kitabu The World Book Encyclopedia kinaeleza hivi: ‘Unywele huacha kukua kila unapofikia hatua ya kutokua. Unywele hubaki katika kitundu cha kutokua hadi hatua inayofuata ya ukuzi. Unywele hutoka unapokuwa katika hatua ya kutokua, wakati unywele mpya unapoanza kukua na kuusukuma nje ya kitundu.’ Asilimia 85 hadi 90 ya nywele huwa katika hatua ya kukua kwa wakati mmoja, asilimia 10 hadi 15 huwa katika hatua ya kutokua na asilimia 1 katika hatua ya kubadilika kwa unywele.

      [Mchoro]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Ukuzi wa mapema

      Unywele unaokua

      kitundu

      mishipa ya damu

      tezi ya mafuta

      unywele

      Hatua ya kutoka

      Hatua ya kutokua

      Unywele mpya unakua

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki