Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Thamini Uwezo Wako wa Pekee
    Amkeni!—2011 | Mei
    • Mkono wa Mwanadamu

      Mikono yetu ni vifaa maridadi vinavyoweza kufanya mambo kwa ustadi wenye kustaajabisha. Tunaweza kuitumia kupitisha uzi kwenye tundu la sindano au kutumia shoka, tunaweza kuchora au kucheza piano. Pia mikono yetu inatambua vitu upesi sana. Kwa kugusa tu tunaweza kutambua ikiwa kitu kina manyoya, ikiwa ni karatasi, ngozi, chuma, maji, au mbao. Naam, mikono yetu haitumiwi tu kushika. Inatusaidia pia kutambua mambo kuhusu mazingira yetu. Nayo inatusaidia kuwaonyesha wengine kwamba tunawapenda.

      Kwa nini mkono wa mwanadamu una uwezo mkubwa hivyo wa kufanya mambo na kugusa? Kuna sababu nyingi. Tuchunguze sababu nne.

      1. Mikono yetu miwili ina zaidi ya mifupa 50 kwa ujumla, na hiyo ni karibu robo ya mifupa yote mwilini. Sehemu mbalimbali za mkono—mifupa, viungio, kano—hufanya mkono wa mwanadamu uwe na uwezo wa ajabu wa kunyumbulika.

      2. Mkono una kidole gumba ambacho kinaweza kugeuka na kugusa vidole vingine vyote vya mkono uleule kwani kimeunganishwa kwa kiungio cha aina fulani ya pekee. Kiungio hicho pamoja na misuli na tishu nyingine hufanya kidole gumba kiwe na nguvu na kiweze kunyumbulika kwa njia ya ajabu.

      3. Mkono huongozwa kwa misuli ya aina tatu. Ile yenye nguvu zaidi—ya mpanuko na ya kunyumbulika—inapatikana katika sehemu ya mkono kati ya kiganja na kiwiko na huongoza vidole kupitia kano. Ikiwa misuli hiyo ingepatikana kwenye kiganja, kiganja kingekuwa kikubwa sana na ingekuwa vigumu sana kukidhibiti! Aina ya tatu ya misuli ni midogo zaidi na inapatikana kwenye kiganja na hivyo kusaidia vidole kutenda kwa njia hususa.

      4. Vidole vyako vina uwezo mkubwa sana wa kuhisi—eneo dogo sana kwenye ncha ya vidole ina vipokezi 2,500 hivi. Isitoshe, vipokezi hivyo vinatofautiana, kila kimoja kikifanya kazi tofauti, kukuwezesha kuhisi wororo wa kitu, joto, umajimaji, kitu kinapotetemeka, shinikizo, na maumivu. Kwa sababu hiyo, kidole cha mwanadamu ndicho kitu chenye uwezo mkubwa zaidi wa kuhisi.

  • Thamini Uwezo Wako wa Pekee
    Amkeni!—2011 | Mei
    • [Mchoro/​Picha katika ukurasa wa 5]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Mifupa tata

      Kiungio kinachotendesha kidole gumba

      Eneo la kudhibiti misuli

      Uwezo wa hali ya juu wa kuhisi

      [Picha]

      Ni nini kinachoiwezesha mikono yetu kufanya mambo mengi sana?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki