-
Usingizi Ni Starehe Tu au Ni Muhimu?Amkeni!—2003 | Machi 22
-
-
Wakati wa usingizi mzito (kipindi cha 3 na cha 4 cha kutosogeza macho), shinikizo letu la damu na mpigo wa moyo hupungua zaidi, na hivyo kupumzisha mzunguko wa damu na kumwepusha mtu na ugonjwa wa moyo.
-
-
Usingizi Ni Starehe Tu au Ni Muhimu?Amkeni!—2003 | Machi 22
-
-
Muhimu kwa Afya
Isitoshe, usingizi huwezesha mwili wetu kuharibu kemikali ambazo inasemekana zinasababisha kansa na kufanya chembe zizeeke. Katika uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Chicago, wavulana 11 wenye afya waliruhusiwa kulala kwa muda wa saa nne tu kwa siku sita. Baada ya kipindi hicho, chembe zao zilifanya kazi kama chembe za watu wenye umri wa miaka 60, na kiwango cha insulini kwenye damu yao kilikuwa kama kile cha mtu mwenye ugonjwa wa sukari! Kukosa usingizi huathiri pia utengenezaji wa chembe nyeupe za damu na homoni iitwayo cortisol, jambo ambalo humfanya mtu apate maambukizo na magonjwa ya damu kwa urahisi.
Bila shaka, usingizi ni muhimu kwa afya ya mwili na ya akili. Kulingana na mtafiti William Dement, mwanzilishi wa kituo cha kwanza cha kuchunguza usingizi katika Chuo Kikuu cha Stanford Marekani, “inaonekana kiwango cha usingizi ambacho mtu hulala ndilo jambo muhimu zaidi ambalo huamua muda atakaoishi.” Deborah Suchecki, mtafiti kwenye kituo cha kuchunguza usingizi huko São Paulo, Brazili, anasema hivi: “Kama watu wangalijua jinsi kutolala usingizi kunavyoathiri mwili, hawangalisema kwamba kulala ni kupoteza wakati au ni uvivu.”—Ona sanduku lililo juu.
-