Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupata Fadhili Zenye Upendo na Utunzaji wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Februari 1
    • Hivyo, tuliwasiliana kupitia barua kwa miezi mitano, kisha nikaenda Hong Kong. Tulioana Oktoba 5, 1965.

      Sote tulitaka kufunga ndoa na kuendelea na utumishi wa wakati wote, na kwa kuwa tulikuwa tunaendelea kuzeeka, tulihisi kwamba tamaa ya kuwa na mwenzi ilikuwa kubwa sana. Nilianza kumpenda Harold na kumheshimu sana nilipoona jinsi alivyotendea watu kwa fadhili na huruma, na jinsi alivyoshughulika na matatizo yaliyohusu utumishi wetu. Tulifurahia ndoa yetu kwa miaka 27 na kupata baraka nyingi kutoka kwa Yehova.

      Wachina ni watu wenye bidii na ninawapenda sana. Huko Hong Kong wanazungumza Canton, lahaja ya Kichina ambayo ni ngumu sana kujifunza kwa kuwa matamshi yake hunyambulika zaidi ya lugha ya Mandarin. Mimi na Harold tulianza maisha yetu ya ndoa katika makao ya mishonari kwenye ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova, kisha tukatumikia katika sehemu mbalimbali za eneo hilo. Naam, tulikuwa wenye furaha sana lakini, mnamo 1976 nikawa na tatizo baya la afya.

      Kukabiliana na Matatizo ya Afya

      Nilikuwa ninatokwa na damu kwa miezi michache, na damu yangu ikapungua sana. Nilihitaji kufanyiwa upasuaji, lakini madaktari kwenye hospitali wakaniambia kwamba hawangefanya upasuaji huo bila damu kwa kuwa kama wangefanya hivyo, ningekufa kwa sababu ya mshtuko. Siku moja madaktari walipokuwa wakizungumzia hali yangu, wauguzi walijaribu kunifanya nibadili nia yangu, wakisema kwamba haikufaa nife bure. Watu 12 walikuwa wafanyiwe upasuaji siku hiyo, na 10 kati yao walikuwa watolewe mimba, lakini nikatambua kwamba hakuna yeyote aliyepinga hatua ya wanawake hao ya kutoa mimba.

      Mwishowe, Harold akaandika barua ya kuiondolea hospitali hiyo lawama iwapo ningekufa, nao madaktari wakakubali kunifanyia upasuaji huo muhimu. Nilipelekwa kwenye chumba cha upasuaji na kutayarishwa kupewa dawa inayomaliza hisia wakati wa upasuaji. Hata hivyo, wakati huo mtaalamu aliyepaswa kunipa dawa hiyo alikataa, hivyo hospitali ikalazimika kuniacha niende nyumbani.

      Ndipo tukaenda kumwona mtaalamu wa magonjwa ya akina mama ambaye hakufanya kazi katika hospitali hiyo. Alipoona kwamba hali yangu ilikuwa mbaya, alisema atafanya upasuaji huo kwa malipo ya chini, maadamu tu tusingemwambia yeyote pesa alizotulipisha. Alifanikiwa kunipasua bila kutumia damu yoyote. Wakati huo, mimi na Harold tuliona wazi utunzaji na fadhili zenye upendo za Yehova.

      Mnamo 1992, Harold aliugua ugonjwa usioweza kupona. Sote tulihamia ofisi ya tawi ambako tulitunzwa kwa upendo. Mume wangu mpendwa aliyekuwa na tumaini la kwenda mbinguni alikufa 1993 akiwa na umri wa miaka 81.

  • Kupata Fadhili Zenye Upendo na Utunzaji wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Februari 1
    • [Picha katika ukurasa wa 26]

      Siku ya arusi yetu huko Hong Kong, Oktoba 5, 1965

      [Picha katika ukurasa wa 26]

      Tukiwa na Wanabetheli wa Hong Kong, Liang na mke wake wako katikati, naye Gannaway na mke wake wako kulia

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki