Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.

  • Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 11. (a) Malaika Gabrieli alimfafanuaje ‘beberu mwenye manyoya mengi’ na ‘pembe yake kubwa’? (b) Ni nani aliyefananishwa na pembe hiyo mashuhuri?

      11 Danieli na hata sisi hatuhitaji kukisia-kisia juu ya maana ya ono hilo. “Yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani [“Ugiriki,” NW]; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza,” malaika Gabrieli amwarifu Danieli. (Danieli 8:21) Mwaka wa 336 K.W.K., mfalme wa mwisho wa Milki ya Uajemi, Dario wa Tatu (Codommanus), alitawazwa. Mwaka uo huo, Aleksanda akawa mfalme wa Makedonia. Historia yaonyesha kwamba Aleksanda Mkuu alikuwa yule ‘mfalme wa kwanza wa [Ugiriki].’ Akianzia “magharibi,” mwaka wa 334 K.W.K., Aleksanda alisonga haraka. Kana kwamba ‘hagusi nchi,’ alishinda maeneo kadhaa na kumpiga dafrao yule “kondoo mume.” Baada ya kuukomesha utawala wa Umedi na Uajemi uliodumu karibu karne mbili, Ugiriki ukawa serikali ya ulimwengu ya tano yenye umaana wa Kibiblia. Ulikuwa utimizo ulioje wa unabii wa Mungu!

      12. Ile “pembe kubwa” ya beberu wa mfano ‘ilivunjwaje,’ nazo zile pembe nne zilizotokea mahali pake zilikuwa nini?

      12 Lakini nguvu ya Aleksanda ilikuwa ya muda mfupi tu. Lile ono laendelea kufunua hivi: “Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.” (Danieli 8:8) Gabrieli asema hivi akiufafanua unabii huo: “Katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.” (Danieli 8:22) Kama ilivyotabiriwa, kwenye upeo wa ushindi wake mbalimbali, Aleksanda ‘alivunjika,’ au akafa, akiwa na umri wa miaka 32 tu. Nayo milki yake kubwa hatimaye ikagawanywa miongoni mwa wanne kati ya majenerali wake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki