Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uzuri na Umaridadi Wenye Kustaajabisha
    Amkeni!—2011 | Aprili
    • Kuwatunza Farasi wa Arabia

      Mfugaji wa farasi wa hali ya juu waliotokana na familia isiyochanganywa chembe za urithi anapaswa kuwatunza vizuri sana. Małgorzata, mmiliki mmoja wa shamba la farasi hao, anaeleza hivi: “Ni jambo tata sana kumtunza farasi wa Arabia. Tunahitaji kumlisha farasi huyo chakula kinachofaa kabisa ili kuhakikisha kwamba anaendelea kuwa na afya bora na kudumisha umaridadi wake. Farasi walio na mimba wanahitaji utunzaji wa pekee hata zaidi.”a Ni chakula gani kinachomfaa farasi huyo wa Arabia?

      Małgorzata anaendelea kusema hivi: “Asubuhi tunaanza kwa kuwalisha nyasi kavu, ambazo huwapa virutubisho vyote wanavyohitaji kutia ndani vitamini na madini. Aina fulani ya shayiri inayoitwa oats iliyochanganywa na makapi au nyasi huwa na virutubisho vingi; pia shayiri na ngano ni vyakula vinavyowafaa. Lakini farasi hao hupenda hasa chakula cha kijani kibichi—nyasi au alfalfa kutia ndani viazi, karoti, na viazisukari. Katika majira ya baridi kali, mara nyingi wazalishaji hununua mchanganyiko wa vyakula vilivyo na protini nyingi. Pia, farasi wa Arabia wanahitaji kuramba chumvi—chumvi huwa na madini au miti-shamba ambayo huwasaidia watulize hasira yao kali. Hata hivyo, lazima isemwe wazi kwamba hata nyasi kavu au chakula bora zaidi kilichonunuliwa hakiwezi kushinda nyasi za malishoni. Na jambo lingine, farasi wanahitaji kupata maji safi ya kunywa kila wakati—hawawezi kunywa maji machafu.”

      Utunzaji wa farasi wa Arabia unatia ndani kushughulikia ngozi na manyoya yake. Hilo linamaanisha wanapaswa kuoshwa kwa uangalifu, kukandwa kwa brashi za pekee, na kupapaswa kwa mikono. Hata hivyo, mengi zaidi yanahusika, kama Tomasz anavyoeleza: “Ni muhimu sana kusafisha kwato zao kila siku, kwa kuwa hilo litazuia wasipatwe na aina mbalimbali za magonjwa, kutia ndani kansa. Lazima pia tuhakikishe tunasafisha macho, mapua, midomo, na masikio ya farasi huyo.” Żaneta anaongezea hivi: “Ili farasi awe na afya na aonekane maridadi anahitaji kukimbia na pia anahitaji mchanga, matope, au nyasi ili agaegae. Anapotokwa na jasho baada ya kukimbia polepole au haraka, kwanza anapaswa kufunikwa kwa blanketi kisha asafishwe baadaye.”

      Wataalamu wanakazia umuhimu wa kumjali kila farasi kihususa. Małgorzata anaeleza hivi: “Inaaminika kwamba farasi wa Arabia wana hisi ya sita—wanapenda kuwa pamoja na mwanadamu, kuguswa na kukumbatiwa. Kutendewa kwa njia hiyo ya kibinadamu humfanya farasi huyo amtumaini yule anayemwendesha hivi kwamba anajitoa kabisa kwa mtu huyo. Imesemwa kwamba wao hutoa sauti wanapoona tabasamu, wanapokumbatiwa, au kulishwa kitu fulani wanachopenda—kama vile karoti au kipande cha sukari. Wale wanaopenda farasi hufurahia sana kuwatunza.” Tomasz anaeleza jinsi anavyowapenda: “Nilivutiwa upesi sana na farasi. Ni wanyama maridadi na wenye madaha ya kipekee. Lakini si rahisi kwao kukuamini. Ilinichukua miaka mingi ili waniamini.”

  • Uzuri na Umaridadi Wenye Kustaajabisha
    Amkeni!—2011 | Aprili
    • [Picha katika ukurasa wa 16]

      Utunzaji wa Kila Siku wa Farasi wa Arabia Unatia Ndani

      1. Kupiga brashi ngozi na manyoya yake kwa uangalifu

      2. Kusafisha kwato zake

      3. Kuwatendea kwa upendo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki