Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Udhibiti Hasira Yako?
    Amkeni!—1997 | Juni 8
    • ULIKUWA mwanzo wenye kuogofya. “Kwa sababu sasa mimi ni kichwa cha nyumba hii, hutaendelea kunisumbua kwa kuchelewa,” John alimpigia kelele Ginger,a bibi-arusi wake mpya. Kwa zaidi ya dakika 45, John aliendelea kumpigia kelele Ginger huku akidai kwamba aendelee kukaa katika kochi. Usemi wenye kuudhi ulikuwa jambo la kawaida katika ndoa yao. Kwa kusikitisha, tabia ya hasira ya John iliendelea kuongezeka. Angebamiza milango, angepigapiga meza ya jikoni, angeendesha gari kama kichaa huku akigongagonga usukani, hivyo akihatarisha maisha ya wengine.

  • Kwa Nini Udhibiti Hasira Yako?
    Amkeni!—1997 | Juni 8
    • Pia, kwa ujumla wanadamu hushindwa kufikiria vizuri matokeo ya baadaye ya hasira zao zisizodhibitiwa. Kunaweza kuwa na matokeo mabaya mtu akishindwa kudhibiti hasira yake. Mathalani, ni matokeo gani ya wazi yawezayo kutokea ikiwa mume ashikwa na hamaki kuelekea mke wake kufikia hatua ya kutoboa ukuta kwa ngumi? Mali inaharibika. Mkono wake waweza kuumia. Lakini zaidi ya hilo, hamaki yake itaathirije upendo na staha ya mke wake kwake? Ukuta waweza kurekebishwa katika muda wa siku chache, na mkono wake waweza kupona katika majuma machache; lakini ni muda gani utakaomchukua kupata tena itibari na staha ya mke wake?

  • Kwa Nini Udhibiti Hasira Yako?
    Amkeni!—1997 | Juni 8
    • Je, John aliyetajwa mwanzoni, aliweza kudhibiti hisia-moyo zake? Je, aliweza kuacha mwendo wake uliomwelekeza kwenye msiba? Kwa kusikitisha, kelele ziliendelea hadi hatua ya kusukuma na kupiga kikumbo. Mashutumu ya kunyoosha kidole cha shahada yaliongoza kwenye midukuo halisi, ya kutia alama na yenye kuumiza. John alikuwa mwangalifu sana kuepuka kukwaruza sehemu za mwili wa Ginger ambazo zilionekana kwa urahisi na alijitahidi kuficha mwenendo wake. Hata hivyo, hatimaye, alianza kupiga mateke, ngumi, kuvuta nywele, na mambo mengine mabaya zaidi. Ginger sasa ametengana na John.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki