-
Je, Dundumio Lako Lina Tatizo?Amkeni!—2009 | Mei
-
-
Dundumio Linapokuwa na Tatizo
Tatizo la dundumio humpata mtu kwa sababu ya kula chakula kisichokuwa na iodini, kufadhaika kimwili au kiakili, kuwa na kasoro katika chembe za urithi, kupatwa na maambukizo, mfumo wa kinga unaposhambulia chembe nzuri, au kupatwa na madhara yanayotokezwa na dawa za kutibu magonjwa mengine.c Dundumio lililovimba, au rovu, linaweza kuonyesha kwamba mtu ni mgonjwa. Uvimbe huo unaweza kuenea katika tezi yote au kutokeza uvimbe mwingine mdogo-mdogo. Ingawa kwa kawaida uvimbe huo si hatari, sikuzote unapaswa kutibiwa kwa kuwa unaweza kuashiria tatizo lingine kubwa, kama vile kansa.d
Kwa kawaida, dundumio lenye tatizo hutokeza homoni nyingi kupita kiasi au chache sana. Kutokezwa kwa homoni nyingi kupita kiasi huitwa hyperthyroidism, kutokezwa kwa homoni chache sana huitwa hypothyroidism. Ugonjwa katika dundumio unaweza kutokea polepole na bila kuonekana, kwa hiyo, mtu anaweza kuwa nao kwa miaka mingi na asitambue. Kama magonjwa mengine, huenda ikawa rahisi kuutibu ukigunduliwa mapema.
Magonjwa ya dundumio yanayowapata watu wengi ni Hashimoto thyroiditis na ugonjwa unaoitwa Graves. Magonjwa yote mawili hufanya mfumo wa kinga ushambulie chembe nzuri ukidhani ni adui. Ugonjwa wa Hashimoto thyroiditis unapatikana mara sita zaidi katika wanawake kuliko katika wanaume, na mara nyingi hufanya dundumio litokeze homoni chache sana. Ugonjwa wa Graves unapatikana mara nane zaidi katika wanawake na kwa kawaida hufanya dundumio litokeze homoni nyingi kupita kiasi.
Kuna maoni mbalimbali kuhusu ni mara ngapi mtu anapaswa kuchunguzwa ikiwa ana ugonjwa katika dundumio, ingawa inasemekana ni muhimu kwa watoto wachanga kufanyiwa uchunguzi kwa ukawaida. (Ona sanduku “Uchunguzi Muhimu kwa Watoto Wachanga.”) Ikiwa uchunguzi unaonyesha kwamba mtu ana dundumio linalotoa homoni chache, kwa kawaida mtu huchunguzwa ikiwa ana chembe zinazoshambulia tezi hiyo. Kwa upande mwingine, iwapo uchunguzi utaonyesha kuwa mtu ana dundumio linalotoa homoni nyingi kupita kiasi, uchunguzi wa ekisirei hufanywa, maadamu mgonjwa si mjamzito au hanyonyeshi. Ikiwa kuna uvimbe katika dundumio huenda sehemu ya uvimbe huo ikakatwa na kuchunguzwa ikiwa ina kansa.
Mtu Anapohitaji Matibabu
Huenda mtu akapewa dawa za kupunguza dalili za kutokezwa kwa homoni nyingi kupita kiasi, kama vile moyo kupiga kwa kasi, kutetemeka kwa misuli, na wasiwasi. Matibabu mengine yanahusisha kuharibu chembe za dundumio ili tezi hiyo itokeze homoni chache. Na nyakati nyingine tezi hiyo inaweza kutolewa.
Huenda daktari akapendekeza wagonjwa walio na tatizo la kutokezwa kwa homoni chache sana au waliotolewa dundumio watumie dawa zilizo na homoni ya T4 kila siku. Ili wawape kiwango kinachofaa cha homoni hiyo, madaktari huwachunguza wagonjwa hao mara kwa mara. Kansa ya dundumio inaweza kutibiwa kwa njia mbalimbali kutia ndani, kupitia madawa, upasuaji, kuingizwa kwa kemikali mwilini, na kupitia miale yenye iodini.
-
-
Je, Dundumio Lako Lina Tatizo?Amkeni!—2009 | Mei
-
-
a Ingawa dundumio linalotoa homoni chache sana linaweza kuhatarisha mimba, wanawake wengi wenye ugonjwa katika dundumio huzaa watoto wenye afya. Hata hivyo, ni muhimu sana kwa mama kupata matibabu ya kuongeza homoni mwilini, kwa kuwa mwanzoni yeye ndiye humpa mtoto wake ambaye hajazaliwa homoni za dundumio.
-
-
Je, Dundumio Lako Lina Tatizo?Amkeni!—2009 | Mei
-
-
d Watu ambao wamepata matibabu ya kichwa na shingo kwa kutumia miale au ambao wamewahi kupata kansa au wenye watu wa ukoo wenye kansa ya dundumio wako katika hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kansa.
-
-
Je, Dundumio Lako Lina Tatizo?Amkeni!—2009 | Mei
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 28]
DALILI ZA KAWAIDA
Hyperthyroidism: Kuudhika sana, kupoteza uzito bila sababu, moyo kupiga kwa kasi, kwenda haja kubwa mara nyingi zaidi, kutopata hedhi kwa ukawaida, kukasirika-kasirika, kuwa na wasiwasi, kubadilika- badilika kwa hisia, kutokeza sana kwa mboni za macho, udhaifu wa misuli, kutopata usingizi, na kuwa na nywele nyembamba zinazokatika haraka.e
Hypothyroidism: Kuwa mvivu na kukosa kuwa makini, kuongeza uzito bila sababu, kukatika kwa nywele, kufunga choo, kuathiriwa sana na baridi, kutopata hedhi kwa ukawaida, kushuka moyo, kubadilika kwa sauti (sauti nzito), kusahau mambo, na uchovu.
[Maelezo ya Chini]
e Huenda dalili nyingine zikasababishwa na magonjwa mengine, kwa hiyo hakikisha unamwona daktari ukijihisi mgonjwa.
-